CCM Tutulize Vichwa, Lowassa ni Tatizo Tulilojitengenezea Wenyewe, Hakujitengeneza-LEMUTUZ - MULO ENTERTAINER

Latest

11 Aug 2015

CCM Tutulize Vichwa, Lowassa ni Tatizo Tulilojitengenezea Wenyewe, Hakujitengeneza-LEMUTUZ

Wamarekani wana Kanuni moja muhimu sana kwenye Rehab zao za kusaidia Wanaotumia Madawa ya Kulevya kwamba kabla ya kuwachukua kwenye Makazi yao ya msaada ni lazima waathirika wajitokeze wenyewe kwenye ofisi za hayo makazi kuomba msaada baada ya kukubali kwa maandishi chini kwamba wana MATATIZO, ndipo wanaweza kupokelewa na kupewa msaada sio vinginevyo. Now wakati umefika CCM tunatakiwa kukubali katika nafsi zetu kwanza kwamba tuna TATIZO na hili tatizo tumejitengenezea wenyewe I mean tatizo la Lowasa kugombea Urais kupitia Upinzani, kuacha mengine yote ya muhimu tuna tatizo moja kubwa sana nalo ni Wananchi wa Tanzania wamekosa kuona Upinzani wa kweli toka Mrema aliposhindwa ku-fit the hype aliyo create mwenyewe ambayo sababu yake kubwa ilikuwa hakuwa na elimu kubwa na uzoefu wa siasa kama Lowasa kwa hiyo ndio maana this time around ninasema CCM tuna TATIZO KUBWA kuliko la Mrema. MWalimu Baba wa Taifa hayupo tena kumzima Lowasa kama alivyomzima Mrema, this time tunatakiwa tuungane na kuwa kitu kimoja tupigane kushika Dola. Hapa mjini kuna bendi moja inaitwa FM Academia Wazee wa Ngwasuma ni bendi inayomilikiwa na mtu mwenye akili sana anawajua vizuri sana Wa-Congo kuwa wakipata sifa kidogo ni watu wa kuhama hama so yeye hajawaruhusu kwa Mwanamuziki mmoja kupata sifa individually bila ya bendi nzima na ameajiri wapigaji wengi sana kiasi kwamba hata mmoja asipokuwepo huwezi kujua kuwa kuna dosari ndio maana ni moja ya bendi chache sana hapa Tanzania yenye Wa-congo wengi lakini imeweza kudumu kwa muda mrefu wakiwa pamoja. CCM tulifanya kosa hili kubwa sana la kuruhusu Kiongozi mmoja wa chama chetu akawa almost bigger than chama tukashituka very late now we are about to pay the price ya makosa yetu wenyewe, ndipo ninaposema cha muhimu sio kulaumiana au kuwalaumu wanaotoka hapana ni kukubali kwanza kwamba kuna makosa tumefanya ila kwa sababu CCM ni kubwa kuliko wanaojitoa tutafute majibu mazuri na mazito yenye busara ndani yake bila ya ku panic tuweze kushika tena Dola!!

- LOWASA:-
Kuingia kwake UKAWA kunabadilisha Completely the picture ya siasa zetu kwa sababu kwenye haya maisha hakuna kitu perfect kila kitu kina mapungufu yake so are our politics na hasa our fragile Democracy now Lowasa offers a sweet package kwa wale wote walioumizwa na mapungufu ya Demokrasia yetu hasa ya ndani ya CCM. UKAWA na Lowasa wana matatizo mengi sana Politically kuelekea Avenue ya kutafuta Urais kwa sababu mpaka sasa hawajaweza kuwachukua kutoka CCM Viongozi wenye Credibility na Public, so far wamechukua Viongozi wengi waliokuwa none effective ndani ya CCM hilo ni la kushukuru sana kwa sababu so far linawasumbua sana na pia kutoka kwa Lipumba na kitendo cha Dr. Slaa kukaa pembeni na ujio wa Lowasa ni pigo kubwa sana kwa UKAWA. Lakini bado Lowasa ni a big threat kwa sababu moja ya pungufu kubwa la CCM madarakani ni Ajira kwa Vijana wengi walioko mijini, ina maana kwamba hawa Vijana wote mjini wasiokuwa na Ajira Lowasa ni jawabu lao sio kwa sababu ana ajira hapana ni kwa sababu ana present a political threat kwa establishment kwa hiyo kwa sababu Vijana hawa hawana anything to lose kwa kumfuata Lowasa aslimia kubwa kati yao watamfuata ingawa wengi wao sio wapiga kura kwa kawaida lakini kwa vile Waziri Mkuu wa zamani wa CCM atakuwa majukwaani anaishambulia CCM it offers excitement kwa Vijana wanaokaa bure bila kazi na huku wameenda Shule. Sio siri kwamba Lowasa atakusanya watu wengi sana kwenye majukwaa yake, ambao watajaa kujionea wenyewe kwa macho yao the history being unfold, pia Wastaafu wa Serikali wengi watamfuata now hawa ni hatari sana kwa sababu ni wapiga kura na wana hasira sana na Serikali ya CCM ambayo kwa mawazo yao haiwajali kwa sababu inawapa penshioni ambayo haikidhi matakwa yao ya maisha the good newz ni kwamba sio wengi isipokuwa kwa kuwa wana tabia ya kuishi sehemu moja kama Kimara sehemu kama hizo ni ngumu sana kwa CCM kukubalika. Viongozi mbali mbali watakaoumizwa kwenye process ya uchaguzi wa sasa wa Kura za maoni watamfuata 20% yao watatuumiza CCM hasa kwenye Serikali za Mitaa na Udiwani na hata kwenye Ubunge, kwenye Urais Lowasa does not present a big threat kwa sababu most of the times of this Campaign atakuwa kwenye ropes kujitetea zaidi kuliko kushambulia on that CCM tunatakiwa kumpa kamba ya kujinyongea yeye mwenyewe ingawa hili linahitaji serious brains behind it. But all and all bado Lowasa anatuletea CCM the best changamoto ever infact this is the fisrt serious challenge CCM we are going to face since our existance 1977, hatuwezi kumchukulia Lowasa kuwa ni poa hapana he is a threat lakini managerable only kama tutatuliza akili chini na kupigana back kistaarabu.

- CCM:-
Ni Chama kikubwa sana na kumekuwepo kabla hata Lowasa hajafikiria kuwa Mwanasiasa, Mwalimu the greatest Leaders ever in the history of our Nation alikuwa ni Binadam mwenye mapungufu pia kwa maoni yangu ni FACT kwamba mapungufu makubwa 2 ya Mwalimu yalikuwa ni SHERIA na UCHUMI na ni matatizo yanayotutesa sana hili Taifa mpaka leo. Mwalimu alikuwa na Tabia ya kuyepeleka mambo ya Kisheria kwenye Kamati Kuu ya CCM badala ya mahakamani, Kiongozi wa Taifa anaharibu Mwanza anahamishiwa Mtwara haya ni mapungufu yaliyoishia kumtengeneza Lowasa our CCM's problem now. Simlaumu Mwalimu kwa sababu Miaka karibu 30 toka Mwalimu apumzike Urais CCM tulikuwa na muda mwingi wa kulirekebisha hili la kulindana ndani ya CCM, lakini tukalipuuzia na kuendelea kushi nalo sasa linataka kutuumiza wenyewe. Pamoja na ukubwa wa political threat ya Lowasa bado sio kubwa sana mpaka akiweza kuwachukua some serious Leaders ndani ya CCM ambao so far ameshindwa ingawa pia kubaki kwa ndani ya CCM wale wote ambao wanajulikana ni wafuasi wake nako kunatuletea tatizo kubwa sana ndani ya CCM.

HOWEVER:- Lowasa na UKAWA, wanapigika tena bila tatizo kwenye uchaguzi only kama CCM ikituliza vichwa chini na kupigana na hili tatizo kwa kutumia akili kubwa na maarifa pamoja na busara kubwa, kwa mfano CCM ni lazima i avoid kupigazana makelele hewa na Lowasa pamoja na UKAWA we should stick to the POLITICAL FACTS. Kwa mara ya kwanza Upinzani watatumia muda mwingi kujitetea kama CCM tukiweza kutengeneza a serious Political Package ya mapungufu ya Lowasa kwa kutumia lugha yao wenyewe Wapinzani ambao wamekuwa mstari wa mbele kwa muda mrefu sana kumshambulia Lowasa akiwa ndani ya CCM. Zipo Video za Viongozi wakuu wa Chadema na UKAWA wakimshambulia Lowasa bila huruma kwamba anatakiwa kunyongwa kutokana na mapungufu yake akiwa Waziri mpaka Waziri Mkuu, now Mwananchi mwenye akili timamu akionyeshwa hizo video bila kuombwa kuangalia kwa matusi na makelele halafu akaonyeshwa tena video za sasa za Viongozi wale wale wa Upinzani wakipigana kumsafisha Lowasa ninaamini mwananchi hatakuwa na tatizo kuamua kati ya CCM na UKAWA nani ni waigizaji wa Sinema na nani ni Chama cha Siasa. CCM tutathimini seriously nani wametoka na effect yao kwenye maeneo waliyotoka na kufanyia kazi matokeo ya tathmini hizo, pia tuwa identify wale wote ambao hawajatoka lakini ni wafuasi wake Lowasa maana hawa ni hatari sana kuliko waliotoka kabisa, tujue wapo wapi, wanafanya nini na namna ya kuwathibiti bila kuanzisha misuguano ambayo ni unnessesary kisiasa. Na kubwa kuliko yote CCM tukatae kata kata kuchukuwa Hostage na hawa wanasiasa mamluki watakao tokea kutaka kujifanya kutaka kutoka ili wabembelezwe kubaki ni muhimu tukajiwekea policy mapema kwamba anayetaka kutoka aende now na hatutambembeleza mtu.

- Wamarekani walilitengeneza tatizo la Binladen alipokuwa tatizo wakaishia kulimaliza wenyewe, halafu wakatengeneza tatizo la General Abacha Nigeria na wakaishia kulimaliza wenyewe, and then wakalitengeneza tatizo la Chief Abiola na wakalimaliza wenyewe, Panama walitengeneza tatizo la Noriega and then wakaishia kulimaliza wenyewe, sisemi tutumia njia zao kumaliza tatizo la Lowasa tulilolitengeneza wenyewe CCM HAPANA, infact uwepo wa Lowasa unatusaidia sana CCM kujibu tuhuma na majungu ya muda mrefu sana kwenye our political arena kwamba kuna Viongozi wa CCM waliokufa kutokana na kutaka kwao kuingia Upinzani. Sababu kubwa ni kwamba kati yao wote hakuna aliyekuwa Mkubwa na mwenye Nguvu kama Lowasa sasa kama CCM huwa ina tabia ya kuwaondoa mbona yupo mpaka leo na anagombea urais kupitia Upinzani? CCM tutulize akili, tujiepushe kujibu jibu makelele ya Lowasa na watu wake kila wakati mengine hayahitaji kujibiwa kabisa kama vile juzi Wasanii walipomuaga Rais JK, Lowasa amepiga kelele hakuna aliyemjibu ila FACTS zilizosemwa na Wasanii wenyewe kwa kusomwa na Msanii Niki wa pili, ile risala imejibu maswali yote ya Lowasa kuhusu Hatimiliki za Wasanii yote Rais JK aliyowafanyia Wasanii toka ashike madaraka mpaka leo anajitayarisha kuyaacha.

- Pia CCM, tukumbuke kwamba kutoka kwa Lowasa na kuingia Upinzani ni good for our Nation Democracy so hata tunaposema sema tuwe tunaweka na akiba ya maneno for the interest of our Nation's Democracy, this is just a test kwa CCM je ni chama kweli cha Mapinduzi na kinachokubalika na wengi kuliko Upinzani? Majibu yake ni rahisi sana lakini only kama CCM itatuliza akili chini na infact CCM bado tunahitaji sana ku explore na kuitumia our biggest political asset yaani Wakinamama, Siasa za Chadema na Upinzani kwa ujumla kwa kawaida hapa Tanzania bado hazijawahi kuwashawishi sana kina mama ambao bado wanaiamini CCM ni wengi na ni wapiga kura. Tumewapoteza Vijana wengi sana kutokana na ukosefu wa ajira lakini the good news ni kwamba Vijana wasio na ajira kwa kwaida sio wapiga kura huwa ni wapiga kelele tu mtaani na kujaa kwenye majukwaa ya Wapinzani.

- Social Media ni muhimu sana kuna wakati Chadema walikuwa wametupiga bao kabisa kwenye hizi area, lakini not now sasa hivi CCM tunawapita kwa at least 10%, kwa sababu converting Lowasa into Chadema bado inawasambua sana operators wao wa Social Media maana it sounds very backwards kulinganisha na jinsi walivyokuwa wanamshambulia sana Lowasa now kwa mara ya kwanza wanajikuta wapo kwenye kamba I mean kwenye kumtetea Lowasa it is a shock itakayowasumbua sana kwa muda huu wa mwanzoni. Now you know kwamba kwenye siasa Kujitetea ni Dalili za kushindwa tayari so CCM tukiwashambulia hawa mapema sana na kuwaweka kwenye kamba kama ilivyo sasa, itawachukua muda sana kurudi kwenye nafasi yao ya zamani ya kushambulia tu huenda wakiamka usingizini Vita itakuwa imekwisha tayari, lakini otherwise bado na wao ni a threat kwa sababu wanasomeka sana mijini ila kama kawaida tunatakiwa kuwajibu with FACTS na safari hii tumepata a golden chance ya kuwashambulia constantly hahahahaha I love it!!

- MUHIMU KULIKO YOTE NI TATIZO LA LOWASA LINATUPA CCM NAFASI YA KUJIKUSANYA KWA PAMOJA TUKIJUA KWAMBA NI TISHIO KWENYE KUSHIKA KWETU DOLA SO NI LAZIMA TUPIGANE PAMOJA KUMSHINDA NA TUTAMSHINDA TU!!

MUNGU AIBARIKI TANZANIA