CHADEMA Wadai wamempa Likizo DR Slaa kwa muda..Ni Kweli ? Wapi Alipo ? - MULO ENTERTAINER

Latest

4 Aug 2015

CHADEMA Wadai wamempa Likizo DR Slaa kwa muda..Ni Kweli ? Wapi Alipo ?

CHADEMA wampa likizo dk Slaa kwa muda....Mbowe aweka wazi kwamba wamekubaliana nae awe likizo nafasi yake katika chama iko pale pale... Kuna mwenye swali mpaka hapo.

Kunani?

Maneno ya Mbowe Haya:

Mbowe-Tumekubaliana na Katibu Mkuu apumzike kwa muda, kwamba sis tuendelee na atakapokuwa tayari ataungana nasi mbele ya safari.

Mbowe-Chama hiki hatukiendeshi kwa siri, tunakiendesha kwa mikakati.

Mbowe-Tulilazimika kutumia kila mbinu halali ambayo inakiwezesha chama chetu kusaka matumaini na matarajio ya wananchi.

Mbowe-Tuliridhika pasipo shaka kwamba ugeni wa Edward Lowassa katika chama chetu ni mpango wa Mungu.

Mbowe-Umoja wetu ndio ushindi, fursa iliyojitokeza ni nadra.

Mbowe-Mtikisiko huu umekuja kwa CCM kipindi ambacho Watanzania wanamatamanio ya mabadiliko

Mbowe-Hatuwezi kuwa chama cha kuendelea kuhubiri mabaya ya jana tukashindwa kuhubiri maendeleo ya kesho

Mbowe- Kipigo wanachopata CCM, hawajawahi kukipata tangu tuanze siasa za vyama vingi

Mbowe-Kila tunayeweza kumpokea kutoka vyama vilivyo nje ya UKAWA tutamchukua

Mbowe-Mungu ameamua kutumia chama chetu kujeruhi na kuangusha CCM.

Mbowe-CHADEMA ni chama cha siasa, ni chama makini, chama makinI ni chama cha watu, chama kisichokuwa makini ni chama cha viongozi.