Kwa masikitiko Makubwa sana, nimemsikia mtoto wa rais wa Kwanza wa Tanzania, hayati baba wa taifa, Makongoro Nyerere siku ya leo pale Jangwani wakati wa uzinduzi wa kampeni za urais za CCM akitoa kauli za kejeli, majigambo na vijembe kuhusu Afya ya Edward Lowassa.
Makongoro kwa mbwembwe kabisa na mizaha alikuwa akiwashawishi watu waliokuwa wanamsikiliza pale, wasijaribu kabisa kumchagua Edward Lowassa kwa sababu ni mgonjwa!
Makongoro anadhani ugonjwa wa mtu ni jambo la kufurahia na kushabikia.
Napenda kumkumbusha Makongoro kuwa wakati baba yake(Hayati Mwalimu Nyerere) anampigia kampeni Benjamin Mkapa mwaka 1995 nchi nzima, tayari mwalimu alikuwa ameshagundulika ana ugonjwa wa Kansa ya damu(Leukemia) na wataalamu wake walishamwambia kuhusu Poor Prognosis ya hali hiyo(He was told that, he would die within six years after been diagnosed to have Leukemia). Hakuna mtu alikuwa anajua hilo wakati huo zaidi ya Mwalimu mwenyewe, Daktari wake
binafsi(Professa Mwakyusa) labda na wasaidizi wake wa karibu sana wa Mwalimu. Lakini Mwalimu alionekana kwenye kampeni za CCM 1998 akiwa mwenye Afya njema, Furaha na Uchangamfu mkubwa sana. Kwa kifupi tu, tambua ugonjwa wa mtu ni siri ya mtu binafsi na wala sio jambo la kushabikia au kushangilia.
Makongoro tambua siasa ni hoja, tena hoja zenye nguvu. Utu wa mtu ni jambo la muhimu sana. Chunga sana ulimi wako. Ipo siku mwenyezi Mungu atakufundisha kitu katika hili ulilolisema leo pale Jangwani\
By J Mdakuz
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI