Nanyimwa Haki Yangu ya Tendo la Ndoa Kisa Mimi ni Mwana UKAWA - MULO ENTERTAINER

Latest

17 Aug 2015

Nanyimwa Haki Yangu ya Tendo la Ndoa Kisa Mimi ni Mwana UKAWA

Imepita takribani week tatu tokea mheshimiwa waziri mstaafu ENL ajiunge na UKAWA na kusema ukweli mimi ni mmoja wa watu niliyekuwa natamani na naendelea kutamani mheshimiwa Mamvi ashike hatamu ya urais wa nchi hii tokea akiwa CCM.

Sasa alivyohama CCM na mimi nilihama nae na kuwa Mwana Umoja Wa Katiba ya Wananchi. Tokea hapo shemeji na wifi yenu ameninunia kwa kuwa yeye ni mwana ccm na ni mgombea wa viti maalum mkoa fulani. Sipewi unyumba na ndani hatuongeleshani. Ila majukumu mengine anayatekeleza kama kawaida. Nimejaribu kukaa nae kuongea nae kwa kituo lakini hataki kabisa kuweka maelewano baina yetu.

Na mimi kama mwanaume nahitaji huduma ya mke wangu mpenzi. Hivyo basi wanabodi naombeni ushauri wenu nifanyeje na mimi siwezi kuitema UKAWA.