Lowassa Utusamehe Sisi Wana CCM, ni Kosa Lipi Lisilohitaji Msamaha? - MULO ENTERTAINER

Latest

15 Sept 2015

Lowassa Utusamehe Sisi Wana CCM, ni Kosa Lipi Lisilohitaji Msamaha?

Ndugu wanaCCM wenzangu, huu ni ukweli. Tabia ya ukweli ni kuumiza mioyo ya watu, kama ambavyo hapa wanaCCM wenzangu watakapoumia mioyo yao na kuanza kunitukana.

Ni hivi, nilikuwa mbishi sana na siku zote nimekuwa nikiamini kuwa CCM tutashinda katika uchaguzi mkuu, nimefatilia kwa umakini mkubwa mikutano ya CCM pamoja na mikutano ya UKAWA, kiukweli kabisa CCM TUMEKWISHA.

Lowassa tulikukosea, tulikusingizia mengi na tunafahamu kuwa kuna watu walikuhujumu. Tunakuomba utusamehe urudi nyumbani (CCM). Ni kweli tumefanya makosa lakini adhabu unayotupa hatustahili Lowassa.

Ndugu wana CCM wenzangu popote pale mlipo mjitokeze tumuombe msamaha mheshimiwa Lowassa, mpaka muda huu Lowassa amekwisha chukua nchi, October 25 asubuhi anakabidhiwa na JK.

By MCHUNGUZI HURU/JF