Ninatafakari hatima ya CCM kama Lowassa angekuwa ni mgombea Urais wa CCM - MULO ENTERTAINER

Latest

15 Sept 2015

Ninatafakari hatima ya CCM kama Lowassa angekuwa ni mgombea Urais wa CCM

Kuna mengi sana yamesemwa kuhusu mchakato wa kumpata mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM uliofanikisha kumpata John Magufuli kuwa mgombea Urais.

Kwa kuangalia kwa nje kabla ya kumteua Magufuli, CCM ilikuwa inakabiliwa na hali yenye mashaka na hatari (awkward situation) kuhusu hatima ya Lowassa.

Kwa kuangalia kwa nje, maamuzi yoyote kuhusu Lowassa ndani ya CCM yalikuwa yanaiweka CCM katika wakati wa aina yake kwenye uchaguzi.

Kwa sasa ni zaidi ya mwezi mmoja tokea mchakato wa kumpata mgombea Urais ndani ya CCM umalizike. Katika muda huu majibu ya maswali mengi yameanza kupatikana.

Kwa sasa ninaweza kusema, kama mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM angekuwa ni Lowassa, CCM ingekuwa imeishashindwa kabla hata ya kuanza kampeni za Uchaguzi Mkuu.

Ndani ya mwezi mmoja akiwa CHADEMA, Lowassa ameonyesha udhaifu mkubwa pamoja na kusaidiwa na CHADEMA/UKAWA kulibeba/kulishusha zigo la ufisadi ambalo amelibeba kwa miaka mingi. CCM wasingeweza kuhimili hoja kutoka upinzani huku wakiwa wamebeba zigo lote la ufisadi na hasa ikichukuliwa hata uwezo wa Lowassa ni mdogo katika kuhimili jukwaa la kisiasa achilia mbali afya yake.

Lowassa akiwa mgombea wa CCM asingeweza kusema maamuzi ya kuendelea na mkataba wa Richmond yalitoka kwenye mamlaka ya juu ili kukabiliana na hoja za wapinzani. Wapinzani kama walivyo watu wengine wasingeamini haya maneno mepesi yasiyokuwa na chembe ya ukweli kiutendaji kwa Waziri Mkuu ambaye aliwahi kusema hawajakutana barabarani na Rais Kikwete.

Kuna wapinzani wengi tu wanaamini maneno ya Lowassa ni uwongo lakini kwa vile Mbowe na genge lake amewaletea Lowassa kama mgombea Urais, wanajikuta hawana njia nyingine zaidi ya kumkubali kama mgombea Urais. ndiyo maana kwa sasa kuna hoja ambazo wanadai wanamtumia tu Lowassa ili kushinda uchaguzi mkuu kwa sababu ana nyenzo fedha.

Kukatwa kwa Lowassa na Uthubutu wa kuihama CCM na kujiunga na CHADEMA kumefanya CCM wapumue na kulifanya zoezi la kumpata Rais wa Tanzania lichukue sura nyingine.

Wahenga walisema, Usilolifahamu ni kama...