Nape Amshambulia LOWASSA....Asema ni Fisadi na Hakuna kazi Aliyofanya Bila Kuiba. Kazungumzia Pia Suala La Lowassa Kujinyea - MULO ENTERTAINER

Latest

29 Sept 2015

Nape Amshambulia LOWASSA....Asema ni Fisadi na Hakuna kazi Aliyofanya Bila Kuiba. Kazungumzia Pia Suala La Lowassa Kujinyea

Mjumbe wa Kamati ya Ushindi ya Chama Cha Mapinduzi, Nape Nnauye ametumia dakika takribani 10 kumshambulia mgombea urais kwa kiketi ya Chadema, Edward Lowassa aliyewahi kuwa kada wa chama hicho.

Nape alirusha makombora yake kwa Lowassa jana alipopewa nafasi ya kumnadi mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli katika viwanja vya Samora, mjini Iringa.

Alisema Lowassa ni mwizi na fisadi na kwamba hakuna sehemu ambayo alipewa kufanya kazi katika ngazi za CCM na serikali bila kuiba.

Nape  alidai  kuwa  Lowassa  alishindwa  kukaa  katika  chama  cha  Mapinduzi  kwa  kuwa  hawezi  kufugika...."Lowassa  ni  Kunguru,Hafugiki." Alisema  Nape.

Katika  hatua  nyingine,Nape  alidai  kuwa  Lowassa  aliwanunua  viongozi  wa  ngazi  za  juu  wa  UKAWA  na  CHADEMA  ili  apate  nafasi  ya  kugombea  kupitia  Chadema  ambayo  awali  ilikuwa  ikimuita  fisadi.

Katika  maelezo  yake,Nape  alisema  mbunge  wa  Iringa  mjini,mchungaji Peter Msigwa  ni  miongoni  mwa  walionunuliwa  na  Lowassa  kwa  shilingi  milioni 340.

Nape  amekuwa  akirusha  makombora  kwa  Lowassa  tangu  alipotangaza  uamuzi  wake  wa  kukihama  chama  hicho  na  kujiunga  CHADEMA.

Nape  aliwahi  kunukuliwa  akisema  kuwa  amekuwa  akipamb
ana  na  Lowassa  kwa  miaka 12  ndani  ya  CCM  na  kwamba  mziki  wake  anaufahamu

Hata  hivyo, tangu  alipoanza  kampeni  zake,Lowassa  amekuwa  kimya  bila  kujibu  mashambulizi  ya  Nape  na  viongozi  wengine  wa  CCM,hali  inayomfanya  azidi  kujipatia  umaarufu  mkubwa  zaidi  wa  kiasiasa.

Wakati  Nape  akitumia  muda  mrefu  kurusha  makombora, Lowassa  yeye  alikuwa  Jijini  Tanga  akifanya  mkutano  mkubwa  wa  kampeni  uliolazimika  kukatishwa  kutokana  na  mafuriko  ya  wananchi  kuzidi  eneo  la  mkutano.

Tazama  Video  Hapo  Chini  Kumsikiliza  Nape