TUSKER FANYA KWELI YAWAFIKIA WAKAZI WA TEGETA NA TEMEKE WIKI HII - MULO ENTERTAINER

Latest

24 Sept 2015

TUSKER FANYA KWELI YAWAFIKIA WAKAZI WA TEGETA NA TEMEKE WIKI HII


 Mpenzi wa bia ya Tusker Bi. Naomi Mahela akipokea zawadi yake ya fulana, mfuko pamoja na bia za bure toka kwa balozi wa bia ya Tusker Veronica Mbilinyi (kulia) pale promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani ilipofunga kambi katika kiwanja cha baa ya Family iliyopo Tegeta jijini Dar es salaam. Baa hiyo iliibuka baa ya wiki kwenye promosheni hiyo inayoendeshwa na bia ya Tusker yenye lengo la kuzihamasisha baa mbalimbali za mitaa inayotuzunguka kufanya kweli kwenye utoaji huduma kwa wateja. Promosheni hiyo inaendelea pia katika mikoa ya Arusha, Mwanza, Moshi, Morogoro na Mbeya. (Kulia) ni Mtangazaji wa redio Efm na mshereheshaji wa promosheni hiyo Gadner Habash.


Mkazi wa Tegeta Kibaoni Goodluck Kagoma (katikati) akipokea zawadi yake ya mfuko, fulana pamoja na zawadi ya bia toka kwa balozi wa bia hiyo Veronica Mbilinyi (kulia) wakati wa wa hafla ya kuipongeza baa ya Family iliyopo Tegeta jijini Dar es salaam ambapo promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani ilifunga kambi siku ya Ijumaa katika kuipongeza baa hiyo iliyoibuka baa ya wiki kwenye promosheni hiyo. (Kushoto) ni Mshereheshaji wa promosheni hiyo na mtangazaji wa redio E-fm Gadner Habash.



Mkazi wa Temeke Maimuna Seif akiifurahia zawadi yake ya fulana toka kwa Afisa Masoko anayejifunza kwa vitendo toka Kampuni ya bia ya Serengeti Bw. Josephat Shelukindo katika hafla ya kuipongeza baa ya Kisuma iliyopo Temeke jijini Dar baada ya baa hiyo kuibuka mshindi wa wiki kwenye promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani Kiwanjani inayodhaminiwa na bia ya Tusker toka Kampuni ya bia ya Serengeti. Promosheni hii ya Tusker imejikita katika kuziunga mkono baa mbalimbali za mitaa inayotuzunguka ili kuhakikisha kuwa zinatambulika kwa wateja wa eneo husika na kufanya kweli kwenye utaoji wa huduma.



Mkazi wa Tegeta Kibaoni na mpenzi wa bia ya Tusker Bi. Leonarda Shayo akiifurahia zawadi yake ya mfuko na fulana aliyokabidhiwa pale promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani ilipofunga kambi ndani ya baa ya Family iliyopo Tegeta jijini Dar. Baa hiyo iliibuka mshindi wa wiki wa promosheni hiyo ambayo inadhaminiwa na bia ya Tusker toka Kampuni ya bia ya Serengeti. Akikabidhi zawadi hiyo (Kulia) ni Balozi wa bia ya Tusker Veronica Mbilinyi na (Kushoto) ni mshereheshaji wa promosheni hiyo Gadner Habash.


Mpenzi wa bia ya Tusker ambaye pia ni mkazi wa jiji la Mbeya Monalisa Makangila(Katikati) akipokea zawadi ya fulana na mfuko toka kwa balozi wa bia ya Tusker Veronica Mbilinyi (Kulia) wakati wa promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani katika baa ya Kisuma iliyopo Temeke jijini Dar. Baa hiyo iliibuka mshindi wa wiki wa promosheni hiyo inayoendeshwa na bia ya Tusker toka Kampuni ya bia ya Serengeti. (Kushoto) ni mshereheshaji wa promosheni hiyo na mtangazaji wa redio Efm Gadner Habash.