Nipo jimboni Bunda wiki ya 2 sasa mambo yangu ya kimajukumu, nimebahatika kutembelea maeneo tofauti tofauti katika jimbo hili. Hali ya kisiasa iliopo kwa sasa Mh.Wassira anaetetea kiti chake anapata wakati mgumu kutokana na kundi kubwa la vijana kumkubali mh. Ester Bullaya na kiuhalisia jimbo hili lina vijana wengi kuliko wazee na kina mama.
Kibaya zaidi kumekuwa na vikesi vya kumpeleka polisi huyu mwanadada Ester Bullaya na baadae kutolewa maamuzi na kuonekana ameshinda mfano kesi ya gari yake. Hivi vitu vimekuwa vikimuongezea umaarufu na kukubalika zaidi na kuonekana bora zaidi kuliko mh. Steven Wasira.
Chama cha mapinduzi (CCM) na Wassara mwenyewe wana siku 20 na ushee kubadilisha upepo uliopo sasa la sivyo heshima uliojijengea kwenye utumishi wako nchi hii zaidi ya miaka 20 itaporomoka kwa kushindwa vibaya na mwanadada huyu, kwa kifupi anaenda kukustafisha kwa lazima, kwa lugha ya vijana wanasema unastaafishwa kwa kichapo au kwenye ndondi wanasema umepigwa kwako.
Kila la kheri mzee wetu
3 Oct 2015
New