Collabo ya mwisho ya Diamond Platnumz na msanii wa Kenya ni ile aliyoshirikishwa na Victoria Kimani kwenye wimbo Prokoto alikuwemo Ommy Dimpoz pia.
Akothee na Diamond wakiwa studio
Baada ya hapo, Diamond amekuwa akifanya ngoma na wasanii wa Nigeria, Afrika Kusini na Marekani zaidi. Hata collabo na wasanii wenzake wa Bongo zimekuwa za nadra pia na hivyo kumfanya kuendelea kuwa msanii anayetafutwa zaidi kwa collabo Afrika Mashariki.
Lakini kuna msanii wa Kenya aliyepata nafasi ya kumshirikisha staa huyo na huyo si mwingine zaidi ya Esther Akoth maarufu kwa jina la Akothee.
Akothee na Babu Tale
Muimbaji huyo amekuja nchini kurekodi wimbo huo na Diamond kwenye studio zake za Wasafi Classic, WCB. Wawili hao waliingia kwenye studio usiku wa kuamkia Alhamis hii.
Akothee akirekodi wimbo wake mpya aliomshirikisha Diamond
Hiyo inakuwa collabo ya pili kubwa kwa Akothee kuifanya mwaka huu baada ya hivi karibuni kurekodi wimbo na Flavour wa nchini Nigeria.
Hivi karibuni aliachia video ya wimbo wake ‘Shengerera Mama’ iliyoongozwa na God Father.