Nilichojifunza katika mahojiano ya Tido na Kingunge, ni kwamba mzee huyu anaujasiri, ambao mwanzo sikuujua. Simkubali Lowassa lakini pia siwezi kukubali anyimwe fursa bila kufuta taratibu. Hata hivyo nimejifunza mambo saba ambayo ninapenda kuwashirikisha.
1. Kikwete na kundi lake walitumia hila katika kimtoa Lowassa katika kinyang'iro cha urais ndani ya CCM.
2.CCM iliwadhalilisha wagombea urais ndani ya CCM kwa kuacha kuwasikiliza na kuwahoji.
3. Kikwete na kundi lake walivunja katiba ya CCM makusudi ili kumdhibiti lowassa, na hawakutoa fursa ya kukata rufaa sababu NEC ilikuwa inamkubali Lowassa, na CC inakatiwa rufaa kwa NEC sababu ndio kikao kikubwa.
4. Maguful pamoja na uzuri wake ameingia doa baada kupata fursa hiyo kwa njia ya mizengwe badala ya utaratibu wa chama.
5.Ufisadi wa Lowassa unakosa mashiko kuzungumzwa na CCM, chama ambacho kina dola ndio chenye wajibu kukamata na kupeleka mahakamani.
Hii ina maanisha huenda Lowassa hausiki kabisa na Richmond au kufikishwa kwa lowassa mahakaman ndo mwanzo wa Kikwete kuondolewa kinga ya kutoshitakiwa.
6. Kingunge ni mtu ujasiri sana kwa kitendo chake cha kutafautiana na wenzake endapo taratibu walizojiwekea zikivunjwa. amethubutu kupingana na Nyerere, mtu ambaye ilitaka ujipange kabla ya kufikiria kumpinga.
7. Hili ni la mwisho lakini ni la kwanza katika umuhimu. Kikwete kama mwenyekiti wa CCM amevunja katiba ya CCM.
Pamoja na hayo lazima tujue akili na busara ndio zilizozaa katiba na kanuni zake za uendeshaji, ni wajibu kufuata katiba lakini ni wazimu kudhani KATIBA ni bora kuzidi BUSARA iliyitumika kutengeneza katiba.
Kama ndivyo, ni sawa kiongozi kujitia wazimu na kupindisha vifungu vya katiba, ili mradi afanye hivyo kwa maslahi ya watu wote wanaongozwa na katiba husika. Asulubiwe kwa kuvunja katiba lakini mafanikio ya uvunjaji huo kuyabeza ni ujununi.
Mwalimu Nyerere aliunganisha TANU na ASP kwa kuvunja mkataba wa muungano, lakini alifanya hivyo kwa lengo kuwa na chama cha kitaifa kitakacho tuunganisha sote bila kuzingatia utanganyika au uzanzibar, amefanikiwa katika hili na katu hatuwezi kubeza.
Je, kikwete kavunja katiba ya CCM kwa maslahi ya wanaCCM wote au kwa maslahi yake na mtandao wake? sio mwanaCCM kwa hivyo jibu sina.
Njano5
0784845394
12 Oct 2015
New
mulo
Siasa