Alikiba Atolea Ufafanuzi Post ya ‘Utata’ Aliyoandika Instagram, na Ampongeza Diamond Kwa Ushindi wa AFRIMA - MULO ENTERTAINER

Latest

20 Nov 2015

Alikiba Atolea Ufafanuzi Post ya ‘Utata’ Aliyoandika Instagram, na Ampongeza Diamond Kwa Ushindi wa AFRIMA

Alikiba ametolea ufafanuzi post yake ya Instagram iliyozua mjadala kwa mashabiki mbalimbali wa muziki ambao waliipokea kwa hisia tofauti.

Siku ya Jumatatu Nov.16 Muimbaji huyo wa single mpya ‘Nagharamia’ aliandika, “Asanteni sana najua mmepiga kura sana lakini nilikuja kugundua baada ya kufuatilia kuwa kuna mambo yanaendelea ya watu wanadiriki hata kupoteza pesa zao kwaajili yangu ila nawaomba fans msinielewe vibaya I will always be there for you #hapakazitu #kingkiba,” post ambayo baadae aliifuta.

Kupitia kipindi cha Ala Za Roho cha Clouds Fm na Diva The Bawse, king Kiba amesema kuwa watu walimuelewa vibaya kwenye post hiyo na ndio sababu kubwa ya kuamua kuifuta,

watu walinielewa vibaya mimi nilikua nawaambia mafans wangu, sababu wao ndo wananipigia Kura mimi sikumaanisha kuhusu tuzo walinielewa vibaya” alisema Kiba.

Hata hivyo licha ya kwamba yeye hakushinda kipengele hata kimoja kati ya vinne alivyotajwa kuwania kwenye tuzo za AFRIMA 2015, lakini hakumpongeza hata msanii mmoja wa Tanzania aliyeshinda ambao ni Diamond na Vanessa Mdee. Kusuhu hilo Alikiba alisema,

Siwezi ku-post kitu kuhusu Kushinda Kwao, unajua hakuna uzalendo. watu wangapi wanafanya Vitu vizuri hawapongezwi? Mimi nafanya vingapi? Sisi sio wazalendo…Unajua watu mimi hawanijui Wanahisi kama mimi nina ringa hivi au nina wivu, ila mimi nawapenda wasanii wote pia mziki mzuri” alisema Alikiba.

Alipoulizwa kuhusu uhusiano wake na Diamond ukoje kwa sasa, ndipo alimpongeza Platnumz kwa ushindi wa tuzo 3.

Mimi sina tatizo na Diamond, nasikia kashida tuzo 3, nampongeza Sana sababu tumepata mtu ambaye anatutambulisha kimataifa ni Kitu poa Sana…Mimi na Diamond we are good” alimaliza Alikiba.