Faiza Ally asema huenda ana ujauzito wa mpenzi wake Mmarekani Hivyo Kurudiana na Sugu ni Ndoto - MULO ENTERTAINER

Latest

1 Nov 2015

Faiza Ally asema huenda ana ujauzito wa mpenzi wake Mmarekani Hivyo Kurudiana na Sugu ni Ndoto

Mzazi mwenzake na mbunge wa Mbeya mjini, Sugu – Faiza Ally, amedai kuwa huenda akawa ni mjamzito.

Akizungumza kwenye kipindi cha Friday Night Live cha EATV, Faiza alisema kutokana na hilo hadhani kama ataweza kurudiana na Sugu tena.

Sasa hivi nipo na mpenzi wangu na pengine naweza kuwa na mimba, not sure kwa sababu sijapima,” alisema. “Kwahiyo kurudiana hiyo ni kwenye ndoto tu siyo kitu hata ambacho unaweza kukizungumzia. Sio mpenzi mpya nimekutana naye baada ya mwaka mmoja kuachana na Sugu, sasa hivi tuna kama mwaka,” aliongeza.