Kassim Majaliwa Aidhinishwa na Wabunge Kuwa Waziri Mkuu kwa Kura 258 - MULO ENTERTAINER

Latest

20 Nov 2015

Kassim Majaliwa Aidhinishwa na Wabunge Kuwa Waziri Mkuu kwa Kura 258

Mh. Kassim Majaliwa amethibitishwa na wabunge kuwa Waziri Mkuu mteule kwa kupata kura za ndio 258 sawa na asilimia 73.5% ya kura zote 351 zilizopigwa.

Kura za hapana ni kura 91 sawa na asimilia 25 ya kura zote, na kura zilizoharibika ni 2.

Majaliwa amemshukuru Rais  Magufuli kwa kumwamini na ameahidi kuwatumikia watanzania wote  bila kujali itikadi zao za vyama.