Ifike mahali CCM, kama chama chetu na chama tawala, kijitenge na siasa za ulaghai, uongo na maigizo. Hasa kwenye mambo nyeti ya nafasi za kiuongozi. Tangu Emmanuel Nchimbi alipochukua fomu ya kugombea Uspika wa Bunge la 11, amekuwa gumzo kwa viongozi na wanachama wa CCM. Kuanzia Makao Makuu ya CCM hapa Dodoma hadi Ofisi Ndogo za Lumumba Dar es Salaam, Nchimbi anasemwa kama asiyefaa na kibaraka.
Anakandiwa na kusingiziwa kuwa bado ni mfuasi wa Lowassa pamoja na kushiriki kampeni za Rais Magufuli. Nchimbi anafanyiwa na kusemewa vitimbi. Yote haya ni kuonesha kuwa Emmanuel Nchimbi hatakiwi kuwa Spika. Kwanini alipewa fomu ya kugombea? Hivi bado CCM yetu inategemea 'vijihela' vinavyotokana na kutoa fomu za kugombea nafasi mbalimbali kupitia chama?
CCM ikumbuke kuwa Dr. Kalokola, yule aliyedai milioni moja yake ya fomu ya Urais, amechukua tena fomu ya Uspika. Huyu aweza kuungana na watu aina ya akina Nchimbi kudai hela yao ya fomu za Uspika. Itakuwa aibu kwa CCM zaidi kuliko kwa wagombea husika. Chama kitaonekana ni cha kitapeli,kilaghai na kimaigizo. Waliochukua fomu za Uspika waachwe wapambane kichama na mmoja wao awe mgombea wetu wa Uspika. Majungu hayajengi chama!
By Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
13 Nov 2015
New
mulo
Siasa