Mchezo wa soka umeendelea kuwa miongoni mwa mchezo unaopendwa na watu mbalimbali wa rika tofauti tofauti katika maeneo tofauti tofauti duniani.
Lakini pamoja na hayo kazi kubwa ya kuhakikisha mchezo huu unazidi kupendwa na kuvutia machoni pa watu ni pamoja na uwepo wa wachezaji mahiri,viwanja vya kisasa pamoja na miundombinu ya uhakikka ya kufanya mchezo huo upendeze pindi unapochezwa.
Lakini yote tisa kumi ni uwepo wa kocha mzuri ambaye atatoa mbinu ambazo zitafanikisha uwepo wa mchezo mzuri,lakini pia mbinu zitakazo mfanya mchezaji aonekane kuwa bora zaidi pindi awapo dimbani.
Ifuatayo ni orodha ya makocha bora zaidi katika soka la sasa ambao kutokana na mbinu zao wamezisaidia timu zao kuweza kufanya vema na kucheza soka safi la kuvutia na ushindi.
KOCHA huyu aliajiriwa bila kutarajiwa, na hata msimu wa kwanza ulipomalizika kulikuwa na tetesi kwamba angefukuzwa kazi.
Lakini ametokea kuwa na mafanikio makubwa kwenye msimu wa 2014/15 kwa kutwaa makombe matatu, ikiwa ni mara moja tu kabla ya hapo walifanikiwa hivyo.
Kabla yake, Barca walifanikiwa kupata vikombe vitatu msimu wa 2008/9 chini ya Pep Guardiola ambapo walitwaa kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya, ubingwa wa La Liga na Kombe la Mfalme au Copa Del Rey.
Chini yake, Copa Del Rey lilipatikana baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Athletic Bilbao kwenye fainali iliyofanyika nyumbani Camp Nou, wiki mbili baada ya kutwaa ubingwa wa Liga kutokana na ushindi wa bao 1-0 nyumbani kwa Atletico Madrid, Vicente Calderon.
Keki tamu zaidi ilifuata jijini Berlin walipowasasambua Juventus kwa mabao 3-1 kwenye mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, kwa kupitia wachezaji Ivan Rakitic, Luis Suarez na Neymar.
Huo ulikuwa ubingwa wao wa Ulaya wa mara ya tano, na Enrique ana kila sababu ya kuona fahari kwa mafanikio ya msimu huo.
Msimu huu pia umeanza vyema, ambapo katika mechi tisa tu tayari walishajikusanyia pointi 21 wakitaka kutetea ubingwa na kupambana na ushindani kutoka kwa mahasimu wao, Real Madrid.
Huyu ni kocha aliyetoka Barcelona, na alifanya hivyo baada ya timu yake kufanya vibaya akaamua kukaa mwaka mmoja akipumzika, kuibukia Allianz Arena.
Ikumbukwe kwamba ni msimu wa 2014/15 tu Bayern Munich walitwaa kombe kwa tofauti ya pointi 10.
Hata hivyo Guardiola aliiongoza klabu yake kutolewa nje ya michuano ya Uefa Champions League ‘ UCL’ katika hatua ya nusu fainali msimu uliopita, ambapo walitolewa na klabu yake ya zamani ya Barcelona.
Kwenye Kombe la Ligi pia walitolewa kwenye hatua kama hiyo hiyo na Borussia Dortmund kupitia mikwaju ya penalti.
Msimu huu umeanza vyema wakitaka kurekebisha makosa yao, wakiwa na nguvu ya mabao ya Robert Lewandowski. Walishinda mechi zote 10 za kwanza, huku baadhi wakidai kwamba ubingwa tayari nje nje.
Pamoja na hayo Guardiola anadaiwa kwamba anaweza kuondoka mwisho wa msimu ili ajiunge na Manchester City kwa ajili ya kwenda kuchukua nafsai ya kocha wa sasa wa timu hiyo Manuel Pellegrini ambaye bado hajaushawishi uongozi wa klabu hiyo kwa kazi anayoifanya katika timu hiyo.
Amewaweka vizuri pia katika mwelekeo wa kutwaa ubingwa wa Ulaya. Alipata kuwa kocha bora 2011.
Dunia ilisimama pale Paris Saint-Germain (PSG) walipowafunga Chelsea na kuwaondosha kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) mwezi Machi mwaka huu, na watu walianza kuiona klabu hiyo kama miongoni mwa timu kubwa
Kwa kifupi ni kwamba Blanc na kikosi chake walizoa kila kitu msimu uliopita nyumbani, kwani walitwaa Trophee des Championes (Super Cup) baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Guingamp.
Lakini pia walitwaa Kombe la Ligi walipowafunga Bastia 4-0, kisha Kombe la Ufaransa kwa kuwapiga Auxerre 1-0 katika fainali na kisha ubingwa wa Ligi Kuu ya Ufaransa Ligue 1 kwa tofauti ya pointi nane dhidi ya waliowafuatia Lyon.
Vijana wa Blanc pia wameanza vyema msimu huu wakiwa moto chini na Zlatan Ibrahimovic wao wakienda vyema kwenye Ligi Kuu na pia katika UCL.
Huyu anaitwa profesa wa soka aliyewawezesha Arsenal kutwaa Kombe la FA mara mbili mfululizo na ndio wanalishikilia bado, likiwa ni la pili kwa ukubwa England baada ya ubingwa wa nchi.
Huyu ni kocha veterani kwani amekaa Arsenal mwaka wa 19 sasa, akiongoza kwa kukaa katika klabu moja kwa muda mrefu zaidi England, nchi yenye ligi maarufu zaidi.
Wenger (66) amejikusanyia kikosi chenye mtindo wa aina yake, ubunifu na wachezaji wenye vipaji kama Sanchez, Mesut Ozil na Santi Cazorla, na walitwaa Kombe la FA kwa kuwacharaza Aston Villa 4-0 dimbani Wembley Mei mwaka huu.
Kwa jinsi Ligi Kuu ya England inavyosonga mbele, kuna kila dalili kwamba Arsenal wanaweza kupanda na si ajabu wakachukua ubingwa japokuwa wanaandamwa na majeruhi wengi.
Mmoja kati ya makocha wanaong’aa Ulaya katika kizazi hiki ni Diego Simeone wa Atletico Madrid aliyewawezesha kutwaa ubingwa wa La Liga katika msimu wa mwaka 2013/14 pamoja na kutofanya vema katika msimu wa 2014/15 ambao walimaliza katika nafasi ya tatu.
Walizidiwa nguvu na Barcelona na Real Madrid na msimu huu unaelekea kuwa mgumu hivyo hivyo lakini raia huyu wa Argentina haoneshi dalili za kukata tamaa, bali anakomaa na vigogo hao.
Amekuwa akikuza na kuendeleza vipaji katika klabu hiyo yenye maskani yake katika dimba la Vicente Calderon kwa miaka kadhaa sasa na amekuwa akiwindwa na klabu kadhaa, ikisemekana kwamba hata Chelsea wanafikiria achukue nafasi ya Jose Mourinho.
Mwanzoni mwa msimu wa 2014/15 ni wachache walikuwa wanamuwazia au hata kumjua kocha huyu, lakini alivyowaongoza Juventus kwa mafanikio, ikiwa ni pamoja na kufika fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya, ikiwa ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 12.
Klabu hiyo ilipatwa majanga ya kushushwa daraja kutokana na kashfa ya Calciopoli ya kupanga matokeo na kutinga Old Trafford 2003, Allegri aliwaongoza wachezaji wake kama Andrea Pirlo, Arturo Vidal na Carlos Tevez kuwapiga timu kama Borussia Dortmund na kwa makeke zaidi, Real Madrid kisha kwenye fainali dhidi ya Barcelona jijini Berlin ambapo waliopoteza kwa kufungwa goli 3-1.
Kwa ujumla ulikuwa msimu mzuri kwa ‘bibi kizee cha Turin’ lakini Huenda kupoteza wachezaji watatu niliowataja hapo huu ni moja ya sababu za kuanza msimu wa 2015/16 bila kasi kubwa, wakiwa chini ya nusu ya jedwali la msimamo wa ligi, lakini kuna dalili za kufyatuka na kupanda juu.
Pamoja na hivi majuzi tu kufutwa kazi ya kuinoa Chelsea, alipata kudhaniwa kwamba angekuwa kocha bora kabisa duniani, kutokana na mwelekeo wa mafanikio yake akiwa na Chelsea sasa katika awamu ya pili.
Hata hivyo, ameanguka kwa kiasi kikubwa kutokana na kuanza msimu vibaya kuliko alivyopata kufanya katika awamu zake zote akipoteza mechi bila mpangilio na kuishia kutimuliwa na uongozi wa klabu hiyo kutokana na matokeo mabovu.
Lakini isisahaulike kwamba amefanikiwa kuzoa vikombe kadhaa na kujenga jina kubwa la Chelsea katika awamu zake zote. Alitwaa Capital One Cup kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Tottenham Hotspur dimbani Wembley, lakini pia ubingwa wa England kwa tofauti ya pointi nane wakiwaacha Manchester City nafasi ya pili.
Mourinho anajulikana kwa jinsi anavyowapelekesha wachezaji wake, akiwapa mazoezi na kushikilia nidhamu ambapo msimu wote uliopita walipoteza mechi tatu tu na hapakuwepo hata moja waliyofungwa wakiwa nyumbani Stamford Bridge.
Mreno huyu mwenye umri wa miaka 52 amekuwa akitumia mbinu za aina yake, akichanganya ufundi, nguvu na haiba yake kutisha wapinzani, hasa makocha kabla ya mechi hivyo kuwaathiri wachezaji wa timu pinzani kisaikolojia.
Utawala wa Sevilla kwenye Ligi ya Europa msimu uliopita ulikuwa wa aina yake, ambapo kocha Unai Emery aliwapa ubingwa huo na kuwaingiza moja kwa moja kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu, akiweka historia kwa mara ya kwanza katika mchakato huo.
Sevilla wametwaa ubingwa huo mara nne, nyingi kuliko timu nyingine yoyote katika historia ya mashindano hayo, makombe mawili yakiwa chini ya kocha huyo.
Walitwaa ubingwa msimu uliopita baada ya kuwachapa Dnipro 3-2 kwenye fainali ya kuvutia iliyofanyika jijini Warsaw, Poland, kwa mabao ya Carlos Bacca.
Hata hivyo, msimu huu Bacca ameondoka pamoja na nyota wengine kadhaa, hivyo kufanya kuanza msimu kwa tabu kidogo na kwenye michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya ambapo walikuwa na kibarua kigumu mbele ya Juventus na Man City ambapo hata waliishia katika nafasi ya tatu.
Hata hivyo, nyumbani wamefanya vyema, ikiwa ni pamoja na ushindi dhidi ya Barcelona. Bado yupo chini kidogo akilinganishwa na majina mengine makubwa ya makocha hadi atakapopata mafanikio mfululizo na timu yake.
10. Carlo Ancelotti (Real Madrid, alifukuzwa Mei)Kutokana na Real Madrid kumaliza katika nafasi ya pili kwenye La Liga msimu wa 2014/15, kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya katika nusu fainali na kuishia hatua ya 16 bora kwenye Copa Del Rey, kupoteza pia mechi ya fainali ya Super Cup, Carlo Ancelotti alifukuzwa kazi.
Aliondoka Santiago Bernabeu Mei mwaka huu, lakini ukiwa ni mwaka mmoja tu tangu awapatie ubingwa wa Ulaya.
Kwa sasa Mtaliano huyo yupo benchi, hana kazi kutokana na Real kutokuwa na subira. Alikuwa akihusishwa na kujiunga Liverpool lakini nafasi hiyo imechukuliwa na Mjerumani Jurgen Klopp.
Huenda hataajiriwa tena kufundisha timu hadi msimu ujao, lakini amekuwa akihusishwa pia na Chelsea, kwani ni kocha mzuri, mwenye umri unaofaa na amejikusanyia mafanikio mengi yaliyotokan na kutwaa mataji yote makubwa Ulaya isipokuwa kombe la Euro akiwa kama kocha.