Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova amepiga marufuku disko toto na milipuko ya baruti katika kusherehekea sikukuu za krismass na mwaka mpya.
Kamanda Kova amesema hayo ikiwa zimebaki siku mbili kusherekea Sikukuu ya Krismasi na siku tisa kusherehekea Sikukuu ya Mwaka Mpya wa 2016 ambazo mara nyingi huwa na shamrashamra na mfululizo wa matukio ya hatari yanayotokana na namna mbaya ya usherehekaji.
Amesema kuwa, anawahakikishia usalama wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wakati wa kusherehekea sikuu za maulidi, krismass na mwaka mpya hivyo wananchi wanatakiwa kusherehekea kwa amani sikukuu hizo.
Kamanda Kova amesema kuwa jeshi hilo litadhibiti wahalifu watakaotumia siku hizo kufanya matukio ya kihalifu na kudhuru watu bila ya sababu.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI