DR Mwaka |
Katika ziara hiyo ilielezwa kuwa Dk. Kigwangwalla aligundua tabibu huyo wa tiba mbadala hakuwa na vyeti lakini taarifa zilizopo zinaonyesha Dk. Mwaka na wasaidizi wake walipewa vyeti kwa mujibu wa sheria na Baraza la Tiba Asilia.
Inaelezwa kuwa Dk. Mwaka amekwisha kukabidhi vyeti hivyo kwa Serikali ikiwa ni kutekeleza agizo alilopewa Desemba 16 mwaka jana na Naibu Waziri Dk. Kigwangwalla.
Dk. Kigwangwalla amekwisha kukiri kuwa vyeti hivyo vimekwisha kufikishwa wizarani na kuhakikiwa.
Kwa sababu hiyo, Mwenyekiti wa Shirikisho la Shirikisho la vyama vya Tiba Asili amesema hatua hiyo ya Dk. Kigwangwalla haikuwa sahihi bali ilisababisha malumbano kwa jamii jambo ambalo si sahihi.
“Hivyo sisi shirikisho tuliweza kukaa na wadau wa Tiba Asili na Tiba Mbadala ambao kimsingi ndiyo hasa walikwazika na agizo hilo la wizara.
“Hatimaye Desemba 31 mwaka jana tulifanya kikao cha pamoja kati ya wadau hao, shirikisho na Wizara ya Afya tukiongozwa na uenyekiti wa Waziri Ummy Mwalimu na kukubaliana baadhi ya mambo lakini si kupiga marufuku matangazo ya tiba mbadala,” alisema Lutenga.
Hata hivyo, Dk. Mwaka alisema hataki kuingia katika malumbano na Serikali na kwa sasa anasukumwa na utoaji huduma kwa jamii kama sheria inavyotaka.
Alisema kutokana na hali hiyo kituo chake kimeandaa utaratibu maalumu wa utoaji matibabu kwa wazee wenye umri wa miaka 60 na kuendelea, pamoja na watoto chini ya umri wa miaka mitano.
Alisema pamoja na misukosuko aliyoipata, Foreplan Clinic pia imejikita kusaidia jamii kama vile ujenzi wa nyumba za ibada ikiwamo misikiti na makanisa na hata kujihusisha masuala ya michezo.