Kimenuka! Mbongo-Fleva mwenye taito kubwa Afrika kwa sasa, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, anadaiwa kutibuana na kaka yake, Romy Jones ‘Romy Jons’, kiasi kwamba hata mawasiliano ya simu hayapo kama ilivyokuwa zamani.
Hivi karibuni chanzo makini kimeliambia gazeti hili kwamba, Diamond na kaka yake huyo ambaye ni mtoto wa mama yake mdogo wamefikia hatua ya kutoongea na hata kuambatana katika kazi zao kama ilivyokuwa mwanzo ambapo Romy Jons ndiye mtu pekee aliyekuwa akipewa nafasi kubwa ya kuwa na Diamond hata katika safari za nje ya nchi.
Imedaiwa kwamba, kisa kikubwa cha wawili hao kugombana ni kufuatia Diamond kushindwa kuendelea kuvumilia tabia za utovu wa nidhamu aliyokuwa akiionesha Romy Jons kila mara, kwani hadi Diamond anafikia hatua hiyo huko nyuma anadai kuiingia hasara kubwa kutokana na kaka huyo kuwa na tabia za ajabu kwani kuna muda alikuwa akimlipia hadi tiketi za ndege ili wasafiri pamoja lakini jamaa akawa hatokei.
Kuna madai kwamba, Romy Jons amekuwa akiambatana na makundi yasiyofaa huku ulevi ukitajwa kuwa tatizo kubwa.
Baada ya kumwagiwa ‘ubuyu’ huo, gazeti hili lilizungumza na Diamond juu ya madai hayo lakini aligusia kwa kifupi kuwa kwenye maisha kila mtu ana namna alivyopangiwa kuishi na Mwenyezi Mungu, hivyo kinachoonekana kwa sasa au kutokuwepo kwa Romy Jons ndani ya Wasafi Classic Baby (WCB) ni mipango aliyochagua Romy Jons mwenyewe kwani yeye hana cha kuongea zaidi.
Alisema kuwa ifahamike kwamba, Romy Jons ni ndugu yake wa damu hivyo dosari au tatizo kati yao linabaki kuwa suala la kifamilia tu.
“Kuna mambo mengine ifikie hatua yaonekane na yapite tu, si kila jambo naweza kuliongelea na kuliweka wazi maana mengine yapo kifamilia zaidi ya watu wanavyochukulia, halafu naomba ieleweke kwamba kwenye dunia hii kila mtu ana namna alivyochagua kuishi, hivyo maisha yangu najua mwenyewe ninavyotamani kuwa kadhalika hata Romy Jons ana mipango yake anayopigania kuikamilisha,” alisema Diamond.
Juhudi za kumpata Romy Jons ziligonga mwamba baada ya simu zake zote kutokuwa hewani hivyo zinaendelea ili kusikia upande wake