Esha Buheti: Nikipata Tatizo Team Diamond Itahusika - MULO ENTERTAINER

Latest

4 Jan 2016

Esha Buheti: Nikipata Tatizo Team Diamond Itahusika

Chokochoko! Msanii wa filamu za Kibongo, Esha Buhet amefunguka kuwa endapo atakumbwa na tatizo lolote basi timu ya Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Team Diamond itahusika.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Esha alisema kuwa chokochoko zilianza alipoposti picha za Ali Kiba mtandaoni ambapo Team Diamond walianza kumtukana na kumwambia watamfanyia kitu mbaya.

Chanzo: Global Publishers Limited