Haya ndio matukio 10 ambayo yatateka hisia za watu wengi wa soka kwa mwaka 2016 - MULO ENTERTAINER

Latest

2 Jan 2016

Haya ndio matukio 10 ambayo yatateka hisia za watu wengi wa soka kwa mwaka 2016

Tayari tumemalizana na mwaka 2015 na sasa tupo katika mwaka 2016, kila mtu anapanga mipango yake katika huu mwaka kuhakikisha kila kitu chake kinatimia. Wakati watu wakiwa wanapanga mipango yao hiyo, katika soka haya ndio matukio 10 ambayo watu wa soka wanasubiri kuyaona yakitokea kwa mwaka 2016.
1- Tuzo ya mchezaji bora wa Dunia Ballon d’Or kwa mwaka 2015 ni moja kati ya matukio yanayosubiriwa kwa hamu kwa mwaka 2016. Tuzo hiyo itatolewa July 11 Zurich Uswissna wachezaji wanaowania ni MessiRonaldo na Neymar.
1
2- Baada ya utawala wa miaka 18 wa Sepp Blatter katika nafasi ya Urais wa shirikisho la soka Ulimwenguni FIFA, mwezi February mwaka huu ndio FIFA itafanya uchaguzi wake wa kwanza bila uwepo wa Blatter na kumpata Rais mpya atakaye mrithi Blatter katika nafasi hiyo.
2
3- Msimu huu umekuwa tofauti sana kwa Ligi Kuu soka Uingereza kutokana na timu kamaLeicester City kufanya vizuri, hivyo ni ngumu kutabiri timu gani itafanya vizuri kwa kutwaa taji hilo msimu wa 2015/2016. Takwimu zinaonesha kuwa ArsenalMan CityLeicester CityTottenham Hotspur na Man United wote wapo katika nafasi ya kutwaa taji hilo, tofauti na miaka ya nyuma mtu ungeweza kutabiri.
3
4- Stori nyingi katika mitandao ya soka barani Ulaya inamuandika kocha wa sasa wa FC Bayern Munich Pep Guardiola kuwa atajiunga na Man City mwezi May na kurithi nafasi ya Manuel Pellegrini baada ya msimu kumalizika, tetesi ambazo zinapata nguvu kutokana kuwa Pep Guardiola tayari amethibisha kutoendelea na FC Bayern Munichmara baada ya msimu kumalizika.
4
5- Baada ya kufukuzwa kwa Jose Mourinho katika klabu ya Chelsea na nafasi yake kuchukuliwa na kocha wa muda Guus Hiddink, wengi wana hamu ya kutaka kufahamu nani atakuwa kocha wa kudumu wa timu hiyo, baada ya msimu wa 2015/2016 kumalizika ila Antonio ConteDiego Simeone wanahusishwa kuwa katika mipango ya Chelsea.
5
6- Jose Mourinho atajiunga na klabu gani baada ya kufukuzwa na Chelsea, ni kweli atakuwa kocha wa Man United kama ambavyo stori zinavumishwa kwa sasa? tusubiri tuone.
6
7- Kuanzia June -July 2016 mashindano ya mataifa ya Ulaya yataanza kutimua vumbi barani Ulaya. Hii itakuwa ni michuano ya 15 kufanyika na itajumuisha jumla ya timu 24. Miongoni mwa timu zitakazo shiriki ni Ujerumani, Hispania, UrenoUbelgijiUingereza,Italia na mwenyeji Ufaransa.
7
8- Mashindano ya Copa America yatakuwa yanafikisha miaka mia moja toka kuanzishwa kwake, hivyo kama hutopenda kuangalia michuano ya Euro unaweza kuangalia michuano hii maalum itakayofanyika U.S.A kwa kushirikisha nchi 10 kutoka Conmebol na timu sita kutoka Concacaf. Hii ni michuano maalum ya kuadhimisha miaka 100 ya michuano hiyo.
8
9- Mwezi August mwaka 2016 kutafanyika michezo ya Olympic ya mpira wa miguu. Michuano hiyo ambayo itahusisha vijana wenye umri chini ya miaka 23, inatajwa kuwa timu za NigeriaAfrika KusiniAlgeriaHondurasMexicoFijiArgentinaDenmark,UrenoSweden na Ujerumani tayari wamethibitisha ushiriki wao katika mashindano hayo yatakayohusisha timu 16.
9
10- Goal Line Technology, hii ni teknolojia mpya katika soka ambayo itaanza kutumika mwezi August 2016, tayari shirikisho la soka barani Ulaya UEFA limethibitisha kuikubali na kuanza kuitumia katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kama hujui mtu wangu kuhusu goal line technology ni teknolojia mpya ambayo itatumika kumsaidia refa kufanya maamuzi sahihi kuhusu mpira kuwa umeingia golini au la.
10
U