LOWASSA Awekwa Mtegoni Kuhusu Urais 2020..Je Ataheshimu Maamuzi ya Chama Kama Asipoteuliwa Kugombea Urais Tena - MULO ENTERTAINER

Latest

21 Jan 2016

LOWASSA Awekwa Mtegoni Kuhusu Urais 2020..Je Ataheshimu Maamuzi ya Chama Kama Asipoteuliwa Kugombea Urais Tena

Kufuatia  kauli ya aliyekuwa mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwavuli wa Ukawa, Edward Lowassa ya kugombea tena urais mwaka 2020, Mkuu wa Oganaizesheni wa NCCR-Mageuzi, Faustine Sungura amemhoji Lowassa kama atakuwa tayari kuendelea kutumikia Ukawa kama jina lake halitapendekezwa kugombea nafasi hiyo.

Sungura amesema kauli hiyo ya Lowassa kupambana tena katika kinyang’anyiro cha urais mwaka 2020 kunategemea maamuzi ya chama kupitisha jina lake.

“Nimemsikia Lowassa anasema kuwa anajiandaa kupambana na Rais John Magufuli mwaka 2020, lakini je, yuko tayari kuheshimu maamuzi ya chama kwa maslahi ya wakati huo?” Alihoji Sungura.