WAKATI wa utawala wa Rais wa awamu ya nne Dr Jakaya Kikwete,moja kati ya jambo alilokuwa akililalamikia kwa sana ni juu ya kukosa uhuru wa kufanya baadhi ya mambo yake binafsi kwa kuwa alikuwa analindwa kila mara.
Dr Kikwete alifikia hatua ya kusema kuwa anatamani amalize muda wake haraka ili apate muda wa kufanya mambo yake bila ya kushirikisha kurugenzi mbalimbali za uchunguzi na utafiti.
Moja kati ya vitu alivyowahi kusema kuwa ‘anavimiss’ ni pamoja na kwenda kucheza dansi pamoja na bao lakini pia alikuwa hawezi kula baadhi ya vyakula kwa kile alichoelezwa kuwa vingeweza kumdhuru.Hali hii ilimfanya Dr Kikwete kufanya baadhi ya mambo kwa kujiiba ,mathalani alijiiba kucheza mziki pindi anapokutana na wasanii ambapo hapo angeweza kukata kiu yake ya kusakata rumba pamoja na wasanii bila ya walinzi wake kumwingilia kwa kuwa hatua hiyo inakuwa miongoni mwa ratiba zinazomtaka yeye kufanya hivyo.Wakati mwingine ambao aliutumia kujiiba toka katika mikono ya walinzi wake ni wakati wa ziara mbalimbali za kitaifa na kimataifa,hapo Jk angeweza kukutana na watu wake wa kitambo na kupiga nao soga muda mfupi kisha kuendelea na ratiba nyingine.
Wakati mwingine pia Jk alitamani kulala hata chini ili tu kukidhi haja yake ya kutaka uhuru wa kufanya kile atakacho kama binadamu wa kawaida,ili kukidhi hayo pia alitumia fursa ya ziara zake mbalimbali kutekeleza mambo kama hayo.Lakini hali hii ni tofauti kwa Rais wa Marekani,Barack Obama ambaye yeye hufanya kila atakacho muda wowote ule ajisikiavyo bila kushurutishwana walinzi wake.Labda tu liwe jambo linaloweza kudhuru maisha yake,hapo angeweza kuongozwa kwanza kisha akaruhusiwa kufanya vile atakavyo.
Hivi hapa ni baadhi ya picha zinazomwonyesha Obama akiwa kajiachia bila kuwepo hata mlinzi wake karibu naye,wakati anakula kile akitakacho na kutmbea na watoto wake katika safari zake za kifamilia