BASATA yaitaka kamati ya Miss Tanzania imalize tofauti yake na kampuni ya Lino - MULO ENTERTAINER

Latest

6 Feb 2016

BASATA yaitaka kamati ya Miss Tanzania imalize tofauti yake na kampuni ya Lino

Baraza la Sanaa la Taifa, BASATA limeitaka kamati ya Miss Tanzania iliyojiuzulu mapema mwaka huu kukaa chini na waandaji wa shindano hilo, Lino Agency kumaliza tofauti zao.

Kupitia Twitter BASATA limeandika:

BASATA imeitaka kampuni ya LINO waandaaji wa Miss Tanzania kurudi mezani na kamati ya shindano kujadiliana namna bora ya kusonga mbele. Imeiagiza LINO kuandaa MoU na kamati ya shindano la Miss Tanzania ili kuchora mipaka ya kiutendaji baina yao.

Kama ya shindano la Miss Tanzania, ilitangaza kujiuzulu kwa kile mwenyekiti wa kamati ya maandilizi ya shindano hilo Juma Pinto, kudai ni kutokana na kushindwa kujua nini majukumu yao na yale ya kampuni inayoyaanda, Lino.

Alidai kuwa awali iliwekwa wazi kuwa ni kamati hiyo ndiyo itakayoratibu mashindano hayo huku Lino Agency ikibaki kuwa washauri.

Pinto alisema Lino imeendelea kufanya kazi yake lakini wao wakibaki bila kujua kinachoendelea. “Sisi tumeona tuje tuzungumze tu kwamba sisi hatupo huko,” amesema Pinto.

Naye msemaji wa kamati hiyo, Jokate Mwegelo alisema kutokana na ukubwa wa kile Miss Tanzania imefanya kwa wasichana, wasilichukulie kwa wepesi na kiubinafsi.

“Waangalie wasichana wa Tanzania wanawatoaje? Na kuwatoa ni kuhakikisha kwanza misingi ya shindano lenyewe iwe ya kueleweka. Kama misingi haieleweki ndio tunarudi kule kule,” amesema Jokate.

Aliongeza kuwa makosa yaliyojitokeza miaka iliyopita pamoja na malalamiko mengi dhidi ya shindano hilo yanapaswa kufanyiwa kazi.