Habari zilizotufikia hivi punde tu zinasema kwamba askari 3 wamefariki dunia huku wengine 3 wawili wakiwa majeruhi na hali zao ni mbaya baada ya kupata ajali mbaya iliyosababishwa na tairi la gari yao iliyokuwa katika msafara wa viongozi wa CCM mkoani Singida kupasuka na kupinduka katika eneo la Mkiwa, wilayani Ikungi.