Mbowe Afunguka Sababu Zilizopelekea Zitto Kabwe Kutochaguliwa Baraza la Mawaziri Kivuli - MULO ENTERTAINER

Latest

7 Feb 2016

Mbowe Afunguka Sababu Zilizopelekea Zitto Kabwe Kutochaguliwa Baraza la Mawaziri Kivuli


Maswali mengi yameibuka hivi karibuni baada ya wadau mbalimbali wa masuala ya siasa kutolisikia jina la mbunge wa kigoma mjini Zitto Kabwe kwa tiketi ya ACT katika Baraza Kivuli la Mawaziri

Mbowe ametoa Ufafanuzi kwanini Zitto Hakuchaguliwa Kama ifuatavyo:

“Ukawa tulisaini tamko la pamoja la ushirikiano na hiyo ilikuwa katika Bunge la Katiba. Kumbuka tumeshirikiana katika Uchaguzi Mkuu na kupata madiwani na wabunge ambao ndiyo hawa wamezaa baraza hili, Ushirikiano wetu upo katika halmashauri na majiji. Kutokana na jambo hilo huwezi kuiingiza ACT maana haikuwapo katika makubaliano ya Ukawa,”


Hata hivyo, baada ya Mbowe kutangaza baraza hilo kivuli, Zitto aliwapongeza na kuahidi kushirikiana nao.