Nay wa Mitego Asababisha Ugomvi Mkubwa Bongo Flava na Bongo Movies... - MULO ENTERTAINER

Latest

4 Feb 2016

Nay wa Mitego Asababisha Ugomvi Mkubwa Bongo Flava na Bongo Movies...

Nay wa Mitego 
Kimenuka! Harufu ya damu inanukia ndani ya tasnia za Bongo Movie na Bongo Fleva, Mbongo Fleva Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ amewachana vibaya mastaa wa filamu ambao nao wameshindwa kuvumilia, wameibuka na kujibu mapigo.

Nay ndiye aliyeanzisha chokochoko za ugomvi huo baada ya kuposti picha yake katika Mtandao wa Instagram na kusindikiza na ujumbe uliokuwa na mlengo wa kuwaponda mastaa wa Bongo Movie, mwishoni mwa wiki iliyopita:

“…Bongo Movie imekufa, wamebaki kuuza sura, wote wanataka kuimba kama Shilole na Snura, Ray Kigo kawa Mkongo mpaka leo anaishi kwao, hela za kuuza muvi zote ananunua mkorogo, kuna Nivar Super marioo, ana gari la milioni kumi, hajawahi miliki hata geto…”

Baada ya kuweka ujumbe huo ambao ulionesha wasanii wa filamu hawana maendeleo, wasanii mbalimbali wa Bongo Movie waliibuka mtandaoni humo na kusema kuwa Nay amechokoza.Wasanii wengine walimjibu kwa matusi huku baadhi yao wakiahidi kumburuza mahakamani.
Kajala Masanja hakuwa nyuma, alifunguka:

“Hivi huyu kwa nini tusimshtaki? Amezidi anajifanya kuponda Bongo Movie wakati hukuhuku ndiyo anafuata wanawake. Anatudhalilisha tumchukulie hatua.”

Jitihada za kuwapata Ray (Vincent Kigosi) na Nivar ili wazungumzie ishu hiyo hazikuzaa matunda baada ya simu zao kuiita bila kupokelewa.

Kwa upande wake Nay alipoulizwa na mwanahabari wetu sababu ya kufanya hivyo, alisema hajutii kuandika maneno hayo kwani yapo kwenye wimbo wake mpya uitwao Shika Adabu Yako ambao ameelezea vitu anavyoamini ni vya kweli.