Ray Kigosi Apigilia Msumari Mwingine kwa Batuli - MULO ENTERTAINER

Latest

6 Feb 2016

Ray Kigosi Apigilia Msumari Mwingine kwa Batuli

Staa wa filamu Vicent Kigosi, maarufu kama Ray ameeleza mustakabali wa filamu yake mpya inayokwenda kwa jina Tajiri Mfupi aliyomshirikisha ndani yake staa wa filamu Batuli ambaye anamtuhumu kwa kutokumlipa chake kwa ushiriki wake ndani ya kazi hiyo.
Ray amesema kuwa, filamu hiyo itatoka kama ilivyopangwa licha ya tuhuma za Batuli, akijitetea kuwa, hawezi kushindwa kumlipa mtu mmoja na kufanikisha kuikamilisha kazi hiyo waliyoifanya miaka 3 iliyopita tayari kwa kuiingiza sokoni.
Ray pia akatolea ufafanuzi hisia zilizoanza kujengeka kuwa, wametengeneza ugomvi huo na Batuli ili kuipatia kiki kazi yao, kitu ambacho amekipinga kwa nguvu.