TRA Yamkalia Kooni Anna Tibaijuka..Yamtaka Alipe Sh Mil 500 Kutoka Katika Mgao wa Fedha za Escrow Alizotafuna.. - MULO ENTERTAINER

Latest

6 Mar 2016

TRA Yamkalia Kooni Anna Tibaijuka..Yamtaka Alipe Sh Mil 500 Kutoka Katika Mgao wa Fedha za Escrow Alizotafuna..


TRA imemtaka Profesa Tibaijuka kulipa zaidi ya Sh. milioni 500 kutoka katika mgawo wa Sh. 1.62 bilioni zinazohusishwa na fedha zilizochotwa katika Akaunti ya Tegeta Escrow

Amepinga madai hayo na kukata rufaa kupinga TRA kumtaka alipe kiasi hicho cha kodi, adai hajawahi kupokea fedha hizo kutoka kwa James Rugemalira.

Inadaiwa kuwa Profesa Tibaijuka, ambaye aliondolewa katika wadhifa wake wa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kutokana na sakata hilo, aliwekewa fedha hizo kwenye akaunti yake na James Rugemalira, Mkurugenzi wa VIP Engineering & Marketing Limited iliyokuwa kati ya wanahisa wa IPTL.

Kutokana na mgawo huo, Desemba 31, 2015, TRA ilimtaka alipe kodi hiyo, baada ya kushindwa kufanya marejesho kutokana na mgawo huo.