Hasira za mafanikio zinatofautiana baina ya mtu mmoja na mwingine. Kama kweli unahitaji mafanikio ya kweli ni lazima uwe na hasira ya njaa kama aliyonayo simba. Miongoni mwetu ni watu wachache sana wanatambua hasira hii ya mafanikio, wengi wetu huchukulia mafanikio kwa sura ya kawaida sana na mwisho wa siku tunaishia kuwa maskini.
Binadamu ni kiumbe wa ajabu sana, nasema hivi ni kiwa na maana ya kwamba binadamu anapenda sana maisha ya kufanyiwa kila kitu, kwa mfano mtu anapenda umpikie chai, umuwekee kwenye chupa, umuwekee chai kwenye kikombe na umgorogee na sukari katika chai na ukishamfanyia yote hayo subiri anywe hiyo chai uone atakavoanza kulaamu utamskia anasema sukari imezidi au sukari hajikolea na lawama zingine nyingi, kitu cha kujiuliza je, mtu huyo alishindwa kuweka sukari mwenyewe kwenye chai yake ili jambo lolote likitokea akose wa kumlamu.
Mtu huyo huyo ukimuuliza unafanya biashara gani? Utamsikia anasema sifanyi biashara yeyote ile mi nipo tu, ukimuuliza kwanini haufanyi biashara yeyote tatizo nini? Atamsikia anakujibu tatizo mtaji huku akiamini kuwa mataji pekee katika biashara ni fedha. Ndugu msomaji wa makala hii hata uwe na fedha kiasi gani kama huna wazo kwa ajili ya matumizi ya fedha, hata ukipewa milioni mia moja leo hizo pesa zitaisha utajikuta mwisho wa siku huna hata mia mbovu. Watu wengi tunatazama mitaji kama fedha peke yake ukitazama katika msingi huo utazidi kulamu mpaka mwisho huku maisha yakiendelea kuwa magaumu.
Ngoja nikuibie siri mtaji unaweza ukaupata kwa kutumia ujuzi pamoja nguvu ulizonazo ili kutengeneza bidhaa au huduma zitazokufanya upate fedha. Kwa mfano Wewe mwenye elimu juu tekinologia ya habari na mawasiliano unaweza ukabili ujuzi wako kuwa bidhaa kwa kuwa fundi wa computer na kutengeza progamu mbalimbali. Swali la kujiuliza unaweza vipi kubadili ujuzi ulio nao kuwa bidhaa au huduma hapo ndipo wengi tunapofeli kwa sababu ni wavivu wa kufikiri.
Naendelea kumchambua binadamu ili uone ni jinsi gani tulivyokuwa na tabia za lawama. Binadamu huyo huyo utamkuta anaishi mazingira machafu ambayo yatasababisha muda wowote magonjwa ya mlipuko kutokea, ukimfuta binadamu huyo na kumuuliza unafikiri ni kwanini mazingira haya ni machafu, utamsikia jibu atakalokupa atakwambia tatizo ni serikali, binadamu huyohuyo utamkuta hana ajira ila ukimuuliza kwanini hauna ajira? Atakujibu tatizo ni serikali.
Kuna msanii mmoja wa hapa nchini aliwahi kuimba kwenye wimbo huku akiuliza serikali ni nini? Maana imekukuwa ikutupiwa lawama kwa kila kitu. Ndugu msomaji wa makala haya nakusihi na kukushauri pia kwa kile ambacho unaweza kukifanya usisubiri serikali ndio ukifanyie, kama unauwezo wa kufanya usafi katika eneo lako fanya usisubiri kuambiwa, maana tabia za bianadamu kwa asilimia kubwa wanasubiri kuambiwa fanya hiki fanya kile . UKisubiri kuambiwa maisha ya mafanikio kwa upande wako yatakuja kwa asilimia chache sana.
Kitu cha msingi ya kuzingatia ni kwamba tuache lawama sizisokuwa na msingi wowote, kwani lawama ulizonazo leo hata yule unayemlalamikia hakusikii na unazidi kuwa maskini tu. Jambo la msingi fanya kila kitu kwa moyo mmoja bila kusubiri mtu fulani akwambie ufanye. Daima tukumbuke usemi huu “kila uonapo nyundo usifikiri kila tatizo ni msumari’’
Mafanikio ya kweli huja kwa mtu kujitambua yeye ni nani? Na ni kwanini upo hapo ulipo. Kuna usemi mmoja hivi wa kiswahili unasema kila binadamu ni mchungaji ,kama ndivo hivyo basi kama mimi leo nikiulizwa nimechunga nini, jibu langu litakuwa lipo wazi ya kwamba natumia muda mwingi kuwafunza watu ili kujua mbinu za kufanikiwa, je wewe mwenzangu unasoma makala hii endapo utaulizwa swali kama hilo utajibu nini? Tafakari kisha uone una thamani gani mbele ya watu wengine?