Hata Kuziba Midomo ni Demokrasia-Rais Magufuli - MULO ENTERTAINER

Latest

24 Jun 2016

Hata Kuziba Midomo ni Demokrasia-Rais Magufuli


Akizungumza leo Ikulu Jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli amewataka wanasiasa waliopewa nafasi za uwakilishi na wananchi wajikite zaidi katika kuwahudumia ili kuwaletea maendeleo waliyowaahidi wakati wa kampeni.

Rais Magufuli amesema kuwa wakati wa uchaguzi umekwisha hivyo wakati wa siasa sasa nao umekwisha hivyo amewataka viongozi wao wa siasa kushirikiana nae katika kuleta maendeleo ikiwemo kumpa ushauri ambao nae ataufanyia kazi kwa maendeleo ya Wananchi wote.

Dkt. Magufuli amesema kuwa kamwe hatomvumilia mtu yoyote ambae atamchelewesha katika harakati zake za kuwaletea maendeleo wananchi, hivyo ni vyema wakaungana kwa pamoja katika kufanikisha suala hilo.

Rais Magufuli amesema wabunge waliochaguliwa waelekeze nguvu katika kuwasemea wananchi kwa kufuata demokrasia ingawa hata kuziba midomo ni demokrasia ya aina yake lakini amevitaka vyama vyote kushirikiana nae katika kulileta taifa maendeleo.