Naibu Spika Amuonya Mbunge wa CHADEMA Baada ya CCTV Kumnasa Akimvua Kofia Mbunge Mwenzake - MULO ENTERTAINER

Latest

25 Jun 2016

Naibu Spika Amuonya Mbunge wa CHADEMA Baada ya CCTV Kumnasa Akimvua Kofia Mbunge Mwenzake



Naibu Spika, Tulia Ackson
Naibu Spika wa Bunge, Tulia Ackson amemuonya Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema) Anatropia Theonest baada ya camera za CCTV za Bunge kumnasa Mbunge huyo akimvua kofia aina ya ‘baraghashia’ Mbunge wa Ulanga (CCM) Goodluck Mlinga aliyokuwa amevaa Bungeni


"Naibu Spika alisema amepitia picha za tukio hilo na amejiridhisha kuwa baada ya kusomwa kwa dua siku hiyo wakati wabunge wa upinzani wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge, Mbunge huyo wa Chadema alipita upande ambao alikuwa amekaa Mbunge Goodluck Mlinga na kumvua kofia na kisha kutoka nayo nje ya ukumbi wa bunge, jambo ambalo lilimfanya kushindwa kuendelea na Bunge kutokana na kutokuwa na vazi rasmi" alisema Naibu Spika

Kanuni za Bunge hazijaweka wazi mwongozo au utaratibu wa kutoa adhabu kwa Mbunge atakayefanya kitendo kama alichofanya Mhe. Anatropia Theonest. Hivyo kwa mamlaka niliyopewa chini ya kanuni ya tano fasiri ya kwanza na kwa kuzingatia matakwa ya kifungu cha ishirini na nne C, D na E cha Sheria kinga na madaraka na haki za bunge natamka kuwa kitendo hicho kilikuwa ni cha dharau kwa kiti cha spika pia kilikuwa kitendo cha fujo ndani ya ukumbi wa bunge. Nachukua hatua ya kutoa onyo kali kwa Mhe. Anatropia Theonest kwamba kitendo alichofanya ni ukiukaji wa sheria na uvurugaji wa shughuli za bunge, hivyo namuonya kwamba asirudie kufanya kitendo kama hicho na endapo atarudia tena hatua kali zitachukuliwa kwa mujibu wa sheria za kanuni za Bunge" alisisitiza Naibu Spika