Shilole na Msanii wake Mpya |
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na video yake ya wimbo ‘SayMyName’, amekiambia kipindi cha Clouds E kinachoruka katika runinga ya Clouds TV, kuwa ameamua kuanzisha label hiyo ili kuwasaidia wasanii wenye vipaji lakini hawapati nafasi.
“Yeah nimemsani Amaselly aka Gaucho, kwa sababu ni msanii mwenye heshima, amenitafuta kwa muda mrefu, Shilole nisaidie nisaidie, kwa hiyo nikajifikiria, nikaamua kumsaidia,” alisema ShilolePia Shilole amesema amemsaini msanii huyo kupitia label yake mpya iitwayo Shilole Entertainment.
Kwa upande wa Amasely alimshukuru Shilole kwa uwamuzi wa kumsaidia huku akihaidi mambo mazuri.
Hii hapa chini ni moja kati ya kazi za msanii huyo ambayo aliifanya kipindi cha nyuma