TID amlalamikia Billnass, ‘sijapenda alikuwa akinibembeleza nimsaidie ajulikane’ - MULO ENTERTAINER

Latest

25 Jun 2016

TID amlalamikia Billnass, ‘sijapenda alikuwa akinibembeleza nimsaidie ajulikane’



Msanii wa muziki na Mkurugenzi wa kundi la Radar Entertainment, TID ameingia kwenye mgogoro na rapper Billnas aliyekuwa member wa kundi hilo kabla ya kutimkia katika label mpya ya ‘LFLG’.

Mapema mwaka huu Billnas aliiambia Bongo5 kuwa aliondoka Rada bila matatizo na mtu yeyote.

Akiongea na Clouds Fm, TID amedai Billnass amesahau alikotoka na hatoi heshima kwa watu walio msaidia kumfikisha hapo alipo sasa.

“Mi sijapenda alikuwa akinibembeleza nimsaidie ajulikane, alikuwa ana nidhamu lakini sasa hivi hanipigii simu, tukimwambia afanye hivi hataki,” alilalamika TID. “Why do we help people who do not help us, why he think he is on top all over the sudden no!! People don’t live like that… People need to respect the people who help u… And of the day,”

Aliongeza, “Mimi i gave out to my heart, my voice, my energy, my talent to make him shine but I don’t see any effort, hajanipa hata laki moja kuniambia nashukuru, anafanya tour hata kuniambia Mzee Mnyama chukua hii laki tano umenifanyia chorus kali neve, huyo mtu wa aina gani hata ungekuwa wewe usingefurahi basi hata shilingi elfu kumi. The first time mimi ndiye niliyemleta Clouds Fm kufanya interview ananiambia siwezi kuongea anatetemeka, ningetaka kumsign halafu ningemmaliza ingekuwa kila napokwenda kufanya shoo angekuwa ananilipa lakini niliona kwamba sina shida kitu nilichokuwa nakihitaji ni ‘appreciation’ ndo maana watu wanatoa cirtificate of ‘Appreciation’,”

Kwa upnde wa Billnas akizungumzia issue hiyo alisema kuwa ameichukulia kawaida kauli hiyo na hajamkimbia TID.

“Mimi natambua mchango wake na nimewahi kuzungumza mara nyingi na najua nafasi yake kwangu na sijawahi kumdharau na kuondoka Radar halitakiwi liwe kosa,” alisema Billnass.