Wabunge wa UKAWA wametoka nje ya Bunge kwa namna tofauti - MULO ENTERTAINER

Latest

20 Jun 2016

Wabunge wa UKAWA wametoka nje ya Bunge kwa namna tofauti

Wabunge wa Kambi ya Upinzani Bungeni leo wametumia mtindo mpya kueleza hisia zao baada ya kuamua kutoka kwenye ukumbi wa Bunge wakiwa wamejifunika midomo kwa karatasi.

Hii ni wiki ya pili mfululizo wabunge hao wamekuwa wakitoka bungeni baada ya kutangaza kutohudhuria kikao cha bunge kinachoongozwa na Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson.

Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia amesema wameamua kutumia mtindo huo mpya kwa sababu Bunge limekataa kuwasikiliza hoja zao.