Zitto Kabwe Amjibu Rais Magufuli Kuhusu Kauli yake ya Kuvitaka vyama vya Siasa Kuacha Kufanya Kampeni - MULO ENTERTAINER

Latest

24 Jun 2016

Zitto Kabwe Amjibu Rais Magufuli Kuhusu Kauli yake ya Kuvitaka vyama vya Siasa Kuacha Kufanya Kampeni

Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe amefunguka na kujibu kauli ambayo ametoa Rais Magufuli kuvitaka vyama vya siasa kuacha kufanya siasa mpaka kipindi cha kampeni tena katika uchaguzi wa mwaka 2020.

Zitto Kabwe ametumia ukurasa wake wa facebook kujibu kauli hiyo kwa kuonyesha kusikitishwa huku na kusema kauli hiyo wao kama wazalendo wanaichukulia kama ni vita dhidi ya demokrasia.
"Tumepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa kauli ya Rais kwamba vyama vya siasa havipaswi kufanya siasa isipokuwa wakati wa Kampeni na kupitia bungeni. Tunaichukulia kauli ya Rais Kama tangazo la vita dhidi ya demokrasia na uhai wa vyama vingi nchini. Chama chetu kitaitisha vikao vya dharura kujadili hali ya nchi na namna ya kukabiliana na mashambulizi yanayoendelea dhidi ya demokrasia nchini mwetu". Aliandika Zitto Kabwe

Mbali na hilo Mbunge huyo aliwataka wanasiasa pamoja na vyama vya siasa kuungana pamoja sasa katika vita hii dhidi ya demokrasia na kuacha tofauti zao ili kuweza kufikia lengo hilo.

"Tunatoa wito kwa Vyama vyote vya siasa nchini kuunganisha nguvu katika kuhakikisha tunapigana vita hii pamoja. Huu ni wakati wa vyama vya siasa na wanasiasa kuacha tofauti zao na kupambana kulinda uhuru wa kufanya siasa wakati wowote kwa mujibu wa Sheria. Tunatoa wito Kwa wananchi wote na taasisi za kiraia kusimama imara Katika Kulinda demokrasia. Tunasisitiza kuwa ushahidi wa kisayansi unaonyesha kuwa huwezi kuua demokrasia bila kuua juhudi za maendeleo. Tusiruhusu mtu yeyote mwenye mamlaka kuua demokrasia nchini mwetu". Alisisitiza Zitto Kabwe