Mwanamuziki Shilole Adaiwa Kumfanyia Figisu Nuh Mziwanda Asiendelee Kimuziki - MULO ENTERTAINER

Latest

30 Jul 2016

Mwanamuziki Shilole Adaiwa Kumfanyia Figisu Nuh Mziwanda Asiendelee Kimuziki

KUNA tetesi kuwa mwanadada asiyekauka kwenye ‘media’ ambaye pia anafanya Muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ amemuundia jeshi aliyekuwa mwandani wake Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ kuhakikisha linamfanyia fujo mara kwa mara ili asiishi kwa amani wala kufanya vizuri kimuziki.

Baada ya tetesi hizo kuenea, Burudani Mwanzo Mwisho (BMM), lilimvutia waya Shilole ili kufungukia madai hayo na alipopatikana ‘aliwaka’ na kudai hataki kumzungumzia Nuh wala hajui lolote kuhusu madai hayo.

“Sihitaji kabisa kuzungumza ishu yoyote kuhusu huyo mtu, niacheni kabisa na wala sifahamu lolote kuhusu madai hayo,” alisema Shilole.

Alipotafutwa Nuh, alisema amesikia ishu hiyo lakini anaamini haitafanikiwa kwani Mungu anampigania.