Baada ya ukaribu wa hivi karibuni wa mwanamitindo Hamisa Mobetto na familia ya Diamond kumekuwepo na sintofahamu kubwa.
Hivi karibuni kulionekana picha ambayo Hamisa amepiga kwenye chumba kile kile ambacho Diamond alilala na mchumba wake, Zari nchini Afrika Kusini.
Kupitia kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM, Diamond aliielezea picha hiyo pamoja na tetesi kuwa na uhusiano na mrembo huyo. “Hamisa nimeanza kumjua zamani sana na sina uhusiano wa kimapenzi na yeye, juzi kati alikuwa kwenye video yangu mpya nimefanya na Ray Vanny na hiyo ndo imeleta maneno maneno yote hayo.”
Na kuhusu picha iliyounganishwa wote wakiwa wametumia chumba kimoja alisema, “Pale ni South Africa sehemu ile inaitwa Capital ni apartment ambazo vyumba vyake vyote vinafanana kama unavyoona hata Madam Rita pia ana share katika hizo apartment naye anayo yake na pia wabongo wengi tunapenda kufikia hapo kidogo huwa ni rahisi.”