Diamond Analipa Fadhila kwa Chid Benz - MULO ENTERTAINER

Latest

7 Aug 2016

Diamond Analipa Fadhila kwa Chid Benz

Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Diamond Platnumz amesema anafanya hivyo kwa Chid Benz kutokana na kitendo alichomuonyesha kabla hajawa maarufu, kukubali kufanya naye collabo ya wimbo wa ‘nalia na mengi’, bila kumzungusha na kumtoza hela kama ilivyo kwa wasanii wengine.

“Mimi nimefanya collabo na Chid, kipindi hicho nilimwambia, hakunitoza hata sh. kumi wala hakunizungusha hata kidogo, ndio maana linapokuja suala la Chidi nakuwa wa kwanza, wakati mimi namfuata Chidi, Chidi hasa nikajua atanikatalia kwanza mimi mbana pua, lakini hakunizungusha na wala hakuniomba hata mia”, alisema Diamond Platnumz.

Tujikumbushe hivi karibuni msanii Chid Benzi alipata matatizo ya matumizi ya madawa ya kulevya, na Diamond alichukua jukumu la kumpeleka hospitali na kumbadilisha damu, kabla hajapelekwa rehab kupata tiba ya urahibu.