Wema Sepetu |
Ameonesha kukasirishwa na baadhi ya watuwanaomsema kwenye mitandao ya kijamii hususani kuhusu mapungufu yake.
Wema Sepetu ametumia mtandao wake wa Instagram kuweka ujumbe mrefu kwa watu hao, huku akiwataka wamuache aishi maisha yake kwani hajawahi hata siku moja kwenda kuomba msaada kwao, na kusema hata siku atakapokufa atakufa mwenyewe na kama ni majibu kwa Mungu atajibu mwenyewe.
“Naomba niseme kitu na nieleweke tafadhari, sijawahi hata siku moja kwenda kwa hata mmoja wenu na kumgongea kuomba hata hela ya chumvi. Maisha yangu yananihusu mimi na hata siku nikifa nakufa mwenyewe, majibu kwa Mungu naenda kujibu peke yangu. Niacheni jamani nimechoka” aliandika Wema Sepetu
Mbali na hilo Wema Sepetu amewataka watu ambao wanakereka na aina ya maisha ambayo yeye anaishi waache kuyafuatilia kwani si lazima kufuatilia kile akifanyacho au maisha anayoishi yeye.
“Kama nakukera na maisha yangu basi usiyafuatilie siyo lazima. Nisiheme sasa jamanii. Naomba tafadhari kama mapungufu ni ya kwangu mimi. Niacheni mimi nafanya kile kinachoridhisha nafsi yangu maana sipendi kujikasirisha. Kwani nikitajirika mimi au nikiwa masikini wewe unapata faida gani. Jiulize kwanza hilo swali ndiyo uanze kutoa maneno yako” alisema Wema Sepetu