Joketi Kujenga Viwanja Vya Michezo - MULO ENTERTAINER

Latest

24 Oct 2016

Joketi Kujenga Viwanja Vya Michezo

Mrembo, Jokate Mwegelo ameahidi kujenga viwanja vya michezo kwa shule ya Sekondari ya Majani ya Chai iliyopo Vingunguti jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika mahafali ya nane ya shule hiyo, Jokate alisema atajenga viwanja hivyo kupitia kampeni yake yake ya kuchangia jamii ijulikanayo kwa jina la “Be Kidotified.”

Amesema ameguswa na changamoto mbalimbali zinazoikabili shule hiyo na kuamua kusaidia kwa kupitia kampeni yake hiyo.

Tayari Jokate amekabidhi viwanja katika shule ya Sekondari ya Wasichana wa Jangwani.