Kwanini Sauti ya Diamond Live ni Mbaya Lakini Nzuri Kwenye Nyimbo Tofauti? - MULO ENTERTAINER

Latest

26 Oct 2016

Kwanini Sauti ya Diamond Live ni Mbaya Lakini Nzuri Kwenye Nyimbo Tofauti?

Jamani mi ni shabiki mkubwa na mzuri wa mziki wa bongo fleva, ila ili jambo linanipa wakati mgumu kuamini, huyu mkali wa bongo fleva diamond ana nyimbo kali sana ila kumekuwa na tofauti kubwa sana katika uwasilishwaji wa nyimbo hizo katika live performance na nyimbo tunazozisikia kwenye radio.

Diamond katika nyimbo ana sauti nzuri yenye base kidogo. Ila huyu jamaa sielewi kwanini akiimba live sauti inakua ingine kabisa yaani mbaya, mbona kina ben paul, banana, kiba king, rayvanny harmonise bela etc wakiimba live sauti inakua ile ile. au kuna ka application kwenye playstore anachokitumia kufanya sauti iwe nzuri studio.

Pia nafikiri sasa diamond aachie kina iyobo kucheza awapo jukwaani yeye afanye kazi moja tu ya kuimba, asijifanye michael jackson, na hii sasa ndo imekuwa weakness ya diamond ambapo mpinzani wake kiba anamfunikia.

Namshauri atafute mwalimu wa sauti na mziki wa live, vinginevyo hatutamuelewa . sauti ya jukwaani cjui ndo yake maana huwa mbaya, na akishindwa kabisa basi bana hata pua bwana

Kwaheri