Nay wa Mitego Adai Wema Sepetu ndiye Aliyemfilisi Idris Sultan (Video) - MULO ENTERTAINER

Latest

27 Oct 2016

Nay wa Mitego Adai Wema Sepetu ndiye Aliyemfilisi Idris Sultan (Video)

Msanii wa muziki wa hip hop Nay wa Mitego ameanza kuitupia madogo kambi ya malkia wa filamu Wema Sepetu kwa kudai mwigizaji huyo ambaye zamani alikuwa mpenzi wa Idris Sultan ndiye aliyemfilisi mshindi huyo wa BBA 2014.

Rapa huyo ambaye yupo kimya kwa sasa, alipost video katika mtandao wake wa instagram akieleza ni kwanini mshindi huyo wa BBA 2014 alifilika.

“Huwa najiuliza kitu kimoja ni mwanamke gani amemaliza mahela ya Idris?,” aliuliza Nay kupitia video hiyo. “Ni yule Msouth au madam (Wema). Mimi nadhani atakuwa madam maana madamu ni mtu wakukwarua mahela mengi, tena kabla hajatua Tanzania walimwambi, huku nyumbani kuna wanawake wacheza sinema maharamia wakikukamata na hizo hela utajikuta huna hata mia,”

Kambi ya malkia huyo wa filamu haijajibu chochote juu ya tuhuma hizo.