Tetesi za Rapper Chemical Kuwa Mapenzini na Producer Wake Maximizer - MULO ENTERTAINER

Latest

15 Oct 2016

Tetesi za Rapper Chemical Kuwa Mapenzini na Producer Wake Maximizer

Rapper wa kike Bongo, Chemical amefunguka kwa kuelezea
sababu inayomfanya afanye kazi nyingi na mtayarishaji wa
muziki  Maximizer.

Akiongea na mtangazaji wa Radio Maisha ya Dodoma,
rapper huyo amesema Max amekuwa akimpatia kwenye
beat zake.

“Nina nyimbo nimefanya na maproducer wengine lakini
nafanya nyimbo nyingi na Maximizer kwa kuwa tumetoka
pamoja kwahiyo nikienda naye mimi nakuwa nasimama na
Max naye anasimama na pia ni mtu ambaye ananipatia sana.
Ninaweza nikaenda kufanya kazi sehemu nyingine lakini
nikiwa na Max nakuwa poa,” amesema Chemical

Rapper huyo ameongeza kuwa hana mahusiano yoyote ya
kimapenzi na Max kama baadhi ya watu wanavyofikiria.