Chris Brown Anyemelea Penzi la Rihanna Upya...Adaiwa Kujipendekeza Kwa Ndugu wa Rihanna - MULO ENTERTAINER

Latest

15 Oct 2016

Chris Brown Anyemelea Penzi la Rihanna Upya...Adaiwa Kujipendekeza Kwa Ndugu wa Rihanna

Chris Brown anaanza kuonekana kama anataka
kurudisha namba ambayo imepotea kwa Rihanna.

Kupitia mtandao wa Hollywoodlife umeripoti kwamba Chris
brown ameanza kuonyesha dalili zote za kurudisha penzi lake
kwa Rihanna baada ya kuonekana kuwa karibu na familia ya
mwanadada huyo kwa kuwatumia zawadi mbalimbali ili
kuonyesha kuwa jina lake lisisaulike katika familia ya
Rihanna.

Kupitia taarifa zilizotolewa chini ya kapeti zimesema
kwamba Chris Brown amerudi tena kwa Rihanna, amemtuma
msaidizi wake Barbados akiwa na vifurushi vyake Rihanna
na familia yake. Ametuma pombe kali, maua na rundo la
midoli kwa ajili ya watoto wote Pia aliweka michoro ambayo
ilikuwa imefunikwa na inaonekana alitengeneza mwenyewe.