Rapper Darassa ameendelea kuweka rekodi mpya katika muziki wake kupitia video yake ya wimbo Muziki ikiwa ni siku 28 toka kazi hiyo iwekwe katika mtandao wa YouTube.
Wimbo huo umemfanya Darassa kuwa juu zaidi katika muziki kwa wakati huu kutokana na wimbo huo kupigwa katika kila kona ya jiji la Dar es salaam pamoja na Tanzania nzima.
Wiki hii video ya wimbo wake huo imefikisha zaidi ya views milioni 2,039,741 ndani ya siku 28 tangu iwekwe kwenye mtandao wa Youtube. Ni nadra sana kwa msanii anayerap kufikisha idadi hiyo ya views katika kipindi hicho.
Wimbo huo kwa muda mfupi umemfanya Darassa awe miongoni mwa wasanii wanaotafutwa sana kwa show wakati huu.