Kinadada washtukia ulaji wa Pweza, 40% wanakula kila siku - MULO ENTERTAINER

Latest

8 Jan 2017

Kinadada washtukia ulaji wa Pweza, 40% wanakula kila siku

Baada ya wanaume kusifika kuwa ndio walaji wakubwa wa minofu ya samaki aina ya Pweza na supu yake, hali sasa imebadilika baada ya kinadada kuonekana pia wakichangamkia kwa wingi kitoweo hicho kinachotajwa kuwa na sifa za kipekee kwa mujibu wa watumiaji.

Inaelezwa kwa wastani kupitia wauzaji waliozungumza na Nipashe imebainika kuwa kuna ongezeko la takribani asilimia 40 ya wateja wanawake anbayo ni  karibu kila kwenye wateja 10 wanaoununua vipande vya Pweza au supu yake kuwa wanne ni wanawake.

Wanaume ndiyo walikuwa wakisifika kwa ulaji wa supu ya Pweza uliopamba moto jijini Dar es salaam katika miaka ya hivi karibuni kutokana na kuwepo taarifa kwamba husaidia mambo mengi mwilini hasa katika kuimarisha urijali kwa wanaume.

UTAFITI WA KITABIBU:
Dr. Damas Mahenda ambaye ni Mhadhiri Msaidizi kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) amesema ni kweli samaki jamii ya Pweza wanafaida nyingi mwili hivyo si ajabu kusikia watu wakichangamkia matumizi yake wakiwemo akina mama.

Dr. Mahenda amesema Pweza wamejawa na virutubisho vinavyosaidia mengi ikiwemo kuongeza hamu na kuboresha tendo la ndoa huku minofu yake ikiwa virutubishpo vya kumuwezesha mwanamke kuwa na sifa halisi za “Ukike” na pia mwanaume kuimarika afya yake.