Imemfikia..na Haya Ndio Majibu:Diamond Afunguka Juu ya Mwanaume Aliyekuwa Anamsumbua Zari,Anasema Alimfanya Hivi Ili Kumkomesha..!!! - MULO ENTERTAINER

Latest

11 Feb 2017

Imemfikia..na Haya Ndio Majibu:Diamond Afunguka Juu ya Mwanaume Aliyekuwa Anamsumbua Zari,Anasema Alimfanya Hivi Ili Kumkomesha..!!!


Pamoja na kumweka ndani na kumzalisha watoto wawili, Tiffah na Nillan, Diamond bado anakumbana na upinzani toka kwa wanaume vichwa nguvu wanaoendelea kujaribu bahati zao ili kumnasa Zari.

Akiongea kwenye kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM Alhamis hii, Diamond alisema baada ya kuona mtu huyo amezidi, alimwambia Zari amchinjie baharini na kudai kuwa hakuwa na uzito wa kumfanya ‘apige simu Kigoma.’

“Kulikuwa na nyendo za mtu mmoja nilishasikia nikasema sasa mambo ya kusumbuana kupiga simu Kigoma tena ya nini. Zari akamblokia zake mbali,” alisema.

“Mwanzo kulikuwa na watu wanaojifanya wao wako karibu sana, kujifanya wao ndio wanamwelekeza ‘Diamond anafanya hivi na hivi.’ Yaani unajua kuna watu wengine wana mambo ya ushamba wanahisi wakikumaliza wanatengeneza nafasi zao. Lakini nikakaa nikasema, kwa suala hili dogo tena mtu mmoja tuanze kupiga simu Kigoma haitakuwa vizuri,” aliongeza.

Hata hivyo Zari na Diamond wamesema wamekubaliana kutoshika simu zao kwakuwa husababisha malumbano makubwa kutokana na wao kuwa watu maarufu.