Askofu Gwajima Afunguka Chanzo cha Utajiri Wake,Adai Analipwa Milioni 2.4 kwa Saa ..!!! - MULO ENTERTAINER

Latest

11 Feb 2017

Askofu Gwajima Afunguka Chanzo cha Utajiri Wake,Adai Analipwa Milioni 2.4 kwa Saa ..!!!




Mchungaji Josephat Gwajima ni mmoja wa watu waliotengeneza vichwa vya habari wiki hii baada ya kutajwa kwenye orodha ya pili ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ya watu wanaotuhumiwa kuhusika kwenye biashara ya madawa ya kulevya.

Gwajima anafahamika kwa utajiri mkubwa kiasi cha kumiliki ndege, helikopta na kudai kuwa na mpango wa kununua treni. Utajiri wake umekuwa ukizusha maswali mengi na kupitia mkutano wake na waandishi wa habari Alhamis hii uliofanyika kanisani kwake, Gwajima alielezea vyanzo vyake vingine vya mapato.

“Cha kwanza mimi ni daktari wa philosophy, ni lecturer peke yake Tanzania kwa malecturer wa kidini ambaye husafiri kwenda kulecture nje ya nchi,” alisema.

“Lecture yangu moja nalipwa dola elfu moja, ambayo ni sawa sawa na milioni 2 na laki kama nne, moja ya saa moja. Nikienda kulecture Japan naweza kulecture miezi mitatu na mimi sijawahi kusafiri na hela mfukoni, hela zote zinakuja kwa benki mpaka hapa. Chini ya kanisa letu kuna kampuni zinaitwa Mahanai Organisations, ni makampuni makubwa.”

Gwajima ametii agizo la kwenda kuhojiwa kwenye kituo kikuu cha polisi jijini Dar es Salaam.