VIDEO: ‘Halima Mdee akamatwe na Polisi hata kwa pingu na aletwe Bungeni’ -Spika Ndugai - MULO ENTERTAINER

Latest

7 Apr 2017

VIDEO: ‘Halima Mdee akamatwe na Polisi hata kwa pingu na aletwe Bungeni’ -Spika Ndugai


Kutokea Bungeni Dodoma Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai ameliagiza Jeshi la Polisi kumkamata na kumfikisha Bungeni Mbunge wa Kawe (CHADEMA) Halima Mdee kujibu tuhuma za kutoa lugha za matusi kwa Spika wakati wa uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki uliofanyika April 4, 2017.
Spika pia amemtaka kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni Freeman Mbowe kufika katika kamati ya maadili, kinga na madaraka ya Bunge siku ya leo kwa ajili ya kujibu tuhuma za kulidhalilisha Bunge.
Full video nimekuwekea hapa chini tayari…